STAA wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ anadaiwa kumzaba makofi mhudumu wa Hoteli ya Lunch Time, Mabibo, Dar aliyetajwa kwa jina la Joyce Mashika.
Joyce aliwaambia wanahabari wetu kuwa Nora alifika hotelini hapo, akaomba chumba na alipoambiwa atoe fedha kwanza aliomba udhamini aingie hotelini kisha atalipa mpenzi wake akifika.
Joyce alidai kuwa walichukua muda wa nusu saa kukubaliana naye lakini baadaye walimpigia meneja wa hoteli ambaye alikubali Nora apewe chumba.
Mhudumu huyo alidai kuwa asubuhi wakati Nora anaondoka, alimzuia na kumdai ile buku tatu na ndipo staa huyo akamzaba makofi huku akimkaba shingoni.
Joyce alisema aliamua kwenda kumfungulia jalada la kesi katika Kituo cha Polisi cha External, Dar kwa jalada namba RB/10153/2013-SHAMBULIO.
Joyce alisema kuwa alishangaa alipofika polisi alikuta Nora ameshafungua kesi akidai kufanyiwa fujo na kuibiwa fedha shilingi laki sita kwenye gari lake ambapo kesi hiyo ilihamishiwa kituo kikubwa cha Mbezi Kwayusuf, Dar lakini Nora hakutokea akiomba
0 comments:
Post a Comment