MWADUI YAITANDIKA TOTO 3-2, VILLA SQUAD WACHAPWA 1-0

TIMU ya Mwadui ya Shinyanga imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya kuifunga Toto Africans mabao 3-2 mjini Mwadui, Shinyanga. Matokeo hayo yanaifanya Mwadui inayofundishwa na kocha na beki wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo itimize pointi 25 baada ya kucheza mechi 12, wakati Toto inabaki na pointi zake 22 katika nafasi ya pili nyuma ya wapinzani wao hao. Mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Rhino imetoa sare ya 1-1 Polisi Mara, Polisi Dodoma imetoa sare ya na 1-1 JKT Oljoro, wakati Villa Squad imefungwa 1-0 na Kimondo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: