ESCROW: IKULU YAZIDI KUMWEKA KIPORO MUHONGO

Licha ya watu mbalimbali kutaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusiana na sakata la fedha za escrow, Ikulu imesema suala hilo litatolewa uamuzi wakati wowote baada ya mapumziko ya sikukuu. Hivi sasa Rais yupo katika mapumziko ya Sikukuu za Krismasi inayosherehekewa Desemba 25 kila mwaka na Mwaka Mpya itakayofanyika Januari Mosi. Akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka huu, Rais Kikwete alisema amemweka kiporo waziri huyo hadi atakapopata ufafanuzi wa mambo kadhaa na kwamba atakapojilidhisha ataujulisha umma. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete bado hajakamilisha kulishughulikia suala hilo na kwamba litakapokuwa tayari wananchi watajulishwa hatua alizozichukua. “Unakumbuka Rais alichosema? Bado analifanyia kazi, atakapomaliza tu mtajulishwa, sasa hivi ni kipindi cha sikukuu,” alisema Sefue. Profesa Muhongo Hata hivyo, Profesa Muhongo alipotakiwa kuzungumzia shinikizo linalotolewa la kutaka ajiuzulu kabla ya Rais Kikwete kutoa uamuzi wake, aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa; “Mimi sasa sitaki kuzungumza na waandishi, mambo yangu yote wapo watu ambao wanaweza kuyazungumzia.” Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Kikwete aliagiza kuchukuliwa hatua kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma kuhusu ushiriki wake kwenye kashfa hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: