Hatua ya 16 Bora – Mchezo wa Pili
Katika mwendelezo wa michuano ya Kuambiana Cup 2025, timu ya Luilo walima nazi imeonyesha ubora wake kwa kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Mbongo wapanda mlima lIkolombogi, katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.
Bao pekee la mchezo lilifungwa na Yusufu Lugongo, ambaye alionesha umahiri mkubwa na kuwapa Luilo ushindi muhimu unaowaweka katika nafasi nzuri kusonga mbele Zaid na nazi zao tamu zaidi.
Matokeo ya Mchezo:
🕹 Full Time
⚽ Luilo 1 – 0 Mbongo
🥅 Mfungaji: Yusufu Lugongo (Luilo)
Kwa ushindi huu, Luilo inasonga mbele kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kusisimua.
Mchezo wa 16 bora wa tatu upapigwa tarehe 29.07.2025 kati ya iwela Wavuvi wa nchi kavu dhidi ya SHUMA kutoka Ngelenge wabishi wa soka katika uwanja wa Masasi
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment