'Ni viwanja vinane vya ndege kati ya 58 ndivyo vyenye hati miliki'


Miongoni mwa viwanja vya ndege nchini kati ya 58
Serikali imeshauriwa  kuhakikisha viwanja vya ndege nchini vinapata hati miliki za ardhi huku kati ya viwanja 58 nchi nzima ni viwanja vinane tu (8) tu ndiyo vyenye hati.
Hayo yamebainika wakati wa utoaji wa taarifa ya mwaka ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu huku ikibaini kuwepo kwa madeni makubwa katika Shirika la Ugavi (TANESCO) kutoka kwa serikali na mashirika yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mjini Dodoma leo, Jumatatu akijibu swali la Mbunge wa Tanga, Mussa Mbarouk lililohusu ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa na wa kisasa katika jiji la Tanga alibainisha hali hiyo.
Mhandisi Ndikiye amesema kuwa kiwanja cha ndege cha Tanga ni miongoni mwa viwanja hivyo 11 vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kugharamiwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa Transport Sector Support Project (TSSP).
"Katika upembuzi huo kiwanja cha ndege cha Tanga ni miongoni mwa viwanja vilivyopewa kipaumbele kwa mahitaji ya ukaribu hivyo katika majadiliano ya awali Benki ya Dunia imeonesha nia ya kugharamia ukarabati wake.”
"Kwa sasa majadiliano kati ya Serikali na Benki ya Dunia yanaendelea yakiwemo mapitio ya awali ya ripoti za miradi iliyopendekezwa pamoja na maandalizi ya taarifa mbalimbali zinazohitajika kabla ya mkataba wa mkopo kusainiwa na baadaye kutangaza zabuni," alifafanua Mhandisi Nditiye.
Hata hivyo, Mhandisi Nditiye alivitaja viwanja vingine vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu  ikiwemo Lake Manyara, Musoma, Iringa, Songea, Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambapo usanifu huo ulimalizika mwezi Juni 2017 kwa kuhusisha usanifu wa miundombinu ya viwanja  hivyo kwa ajili ya upanuzi na ukarabati ili kukidhi mahitaji ya sasa.
Biashara







Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: