Ni jambo unaloweza kuliita ni ajabu ambapo mtoto wa umri wa mwezi mmoja tangu kuzaliwa kuota meno saba na kusababisha Madaktari kumfanyia upasuaji kuyaondoa meno hayo.
Tukio hilo limetokea India ambapo mmoja wa Madaktari waliomfanyia upasuaji mtoto huyo, Meet Ramatriamesema upasuaji umekua na mafanikio baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili; upasuaji wa kwanza ulikua wa kutoa kwanza meno manne na baadaye akatolewa meno matatu.
Wazazi wa mtoto huyo waligundua kuwa mtoto wao hanyonyi vizuri hivyo kuamua kumpeleka Hospitali ili kufanyiwa uchunguzi ndipo madaktari walipogundua mtoto huyo ana tatizo hilo ambapo hata hivyo daktari huyo ameeleza haijulikani kama upasuaji huo utaathiri uotaji wa meno wa mtoto huyo kwa siku za usoni.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment