Haya ni maajabu ya pete ya kuokota yanayomtokea huyu !




ring_sakawaKijana mmoja kutoka Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeanza kupuputika huku nyama za kidole hicho zikionekana kulika.
Kijana huyo Eric Buageng, alisema iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole chake, akaanza kusikia maumivu na pete hiyo ikaanza kumbana kidole.
Eric-Buabeng
Eric Buageng
Eric amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa ukitetemeka, akashindwa kuitupa pia, halafu akasikia sauti ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anasikia sauti ikimwambia atoke nje.
Jitihada zake zimeonekana kutokuwa na matumaini yoyote kwenye mikasa inayomkuta kwenye pete hiyo, ameshaenda Hospitali  na pia kwa wachungaji na hakuna mafanikio yoyote huku wakihisi kwamba pete hiyo ina uhusiano na masuala ya uchawi.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: