Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hautakurupuka kufanya maamuzi ya kumtema mchezaji yeyote katika kipindi hiki cha dirisha dogo hadi utakapopata ridhaa kutoka kwa kocha wao mkuu George Lwandamina.
Mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo Husseni Nyika, ameiambia Goal, kuwa mpaka sasa hawajatangaza kuachana na mchdezaji yeyote na wanashangazwa na taarifa ambazo zina sambazwa kwenye vyombo vya habari ambavyo vinataja baadhi ya majina ya wachezaji waliowaacha.
"Bado hatujafika kwenye zoezi la kuacha mchezaji na sidhani kama tunaweza kufanya hivyo kwasababu Yanga tunakawaida ya kufuata misingi na protoko ambazo zinauelekeza mchezo wa soka lakini pia tunasikiliza sana kauli ya kocha kwasababu yeye ndiyo anayejua vizuri uwezo na mchango wa wachezaji wake,"amesema Nyika.
Kiongozi huyo amesema pamoja na kutangaza kusajili wachezaji wawili mkapa sasa hiyo siyo sababu ya kutaka kutema mchezaji kwasababu kila mmoja wao ananafasi yake ndani ya timu
Yanga tayari imekamilisha wachezaji wawili ambao ni beki Feston Kayembe na Nkomola ambaye alikuwa akiichezea timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 'Ngorongoro' Heroes.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment