Klabu ya Simba imemtangaza mfanyabiashara Mohammed Dewji kuwa mshindi wa zabuni ya asilimia 50 ya klabu hiyo kwa thamani ya Sh20 bilioni.
Klabu ya Simba imemtangaza mfanyabiashara Mohammed Dewji kuwa mshindi wa zabuni ya asilimia 50 ya klabu hiyo kwa thamani ya Sh20 bilioni.
Baada ya kutangazwa, Dewji amesema kuwa ushindi wake ni ushindi wa Simba. "Sidhani kama kuna aliye na shaka juu ya ushabiki wangu juu ya Simba."
Pia ameahidi neema klabuni hapo akisema, "klabu yetu ina miaka 81 lakini hatuna hata kiwanja kimoja cha mazoezi. Tumetenga pesa kwa ajili ya kujenga viwanja viwili vya mazoezi, Mgahawa,Gym na hostel ya wachezaji.
"Tunatarajia kutenga zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya usajili. Pia tunampango wa kufungua kutuo chetu cha TV."
Aliongeza kwa kusema kwamba kwa namna ya pekee, klabu ya Simba inapenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika kujenga Tanzania ya viwanda. “Sisi kama klabu tumeamua kujenga kiwanda kikubwa sana Tanzania, ambacho ni klabu ya Simba Sports Klabu."
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya zabuni, Jaji Thomas Mihayo alisema kwamba tarehe 18 Oktoba, kamati maalum ya uwekezaji ilipokea maombi ya watu waliojitokeza kuwekeza @SimbaSCTanzania . Kamati ilikaa na kutathimini vigezo vilivyowekwa. “Ilipofika mwezi wa kumi mwishoni kamati ilituma mwaliko kwa mwekezaji aliyekidhi vigezo na tulikaa nae na tukaridhika na mipango mikkati yake.”
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment