Asante Kwasi (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania waliokutana msimu huu kwenye dimba la Uhuru DSM na kumalizika kwa sare ya bao 1-1
Uongozi wa Klabu ya Lipuli FC imekanusha taarifa zilizoandikwa katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zinazohusu mchezaji wake Asante Kwasi kujiunga na klabu ya Simba.
Msemaji wa Lipuli FC amesema mchezaji huyo bado ni mali halali ya wanapaluhengo hivyo kama kuna timu imevutiwa ni vyema ikafika katika meza ya mazungumzo na viongozi wa Lipuli badala ya kuishia kuwaaminisha wapenda soka kupitia vyombo vya habari.
Taarifa kuhusu kuondoka kwa Asante Kwasi klabuni hapo zimeripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari zikimnukuu mmoja viongozi wa Simba akidai kuwa wamemaliza taratibu za kumsajili beki huyo raia wa Ghana kwa mkataba wa miaka miwili.
Katika hatua nyingine Lipuli FC imeendelea kuimarisha kikosi chake katika kipindi hiki cha dirisha dogo kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji akiwemo kiungo Salum Machaku ambao nafasi zao zitazibwa na wachezaji ambao wapo katika hatua za mwisho za usajili.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment