kata ya Nkomang`ombe wilayani Ludewa mkoani Njombe wamemlalamikia Afisa mtendaji wa kata hiyo

LUDEWA
Wakazi wa kijiji na kata ya Nkomang`ombe wilayani Ludewa mkoani Njombe wamemlalamikia Afisa mtendaji wa kata hiyo kuwa hawatendei haki kwa kile kilichodaiwa kuwa mtendaji huyo anatumia ofisi hiyo kama ni jengo lake binafsi na siyo jengo la serikali.
Hoja hiyo ilibuka mara baada ya kutokea mvua kali wakati wa mkutano wa kusoma mapato na matumizi ndipo wananchi hao walipo hoji kuwa kwa nini mlango wa ofisi ya kata umefungwa majibu ya uongozi wa serikali ya kijiji pamoja na baadhi ya wajumbe walisema ofisi hiyo imefungwa na mtendaji kata
kwa kuwa ni ofisi yake.
Wananchi hao walionyesha kukerwa na majibu hayo na kitendo ambacho kinafanyika na Afisa mtendaji wa kata ya Nkomang`ombe hasa kufunga ofisi na kuwanyima samani za kutumia kwenye mkutano zikiwemo meza na viti huku wakisema ofisi hiyo ilijengwa na wao kama wananchi na waliendelea kusema mtendaji huyo ameletwa na serikali na ameikuta ofisi hivyo anapaswa kujua ofisi hiyo niya wananchi na siyo yake walisema wananchi hao.
Mara baada ya malalamiko ya wakazi hao na viongozi wa serikali ya kijiji akiwamo mwenyekiti wa kijiji hicho Bw,Steven Haule, best fm redio ilifanikisha kuzungumza na Afisa mtendaji kata Bw,Ezekia Mligo juu ya kulalamikiwa na wakazi wake ambaye alikanusha maneno hayo na kusema wasimtafute kabisa kwa sababu zisizo za msingi badala yake wafanye kazi za maendeleo.
Kwa mara nyingine mkutano huo wa kusoma mapato na matumizi uliahirishwa tena na kupanga ufanyike jumapili ya Decembe 17 mwaka huu kutokana na sababu ziliainishwa hapo juu pamoja na mvua.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: