Yanga ipo katika mazungumzo mazito na mshambuliaji Mtanzania anayecheza soka kwenye klabu ya Dhofar FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman.
Mshambuliaji huyo ameiambia Goal, yupo tayari kurudi Tanzania, lakini endapo Yanga watampatia kitita cha Tsh. 80 Milioni, ili aweze kujiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili.
"Nipo tayari kucheza Yanga, lakini sharti langu kubwa nilazima wanilipe Sh. 80 Milioni ambazo naweza kuvunja mkataba wangu uliobaki wa mwaka mmoja na nusu kule Oman ili nije kuwatumikia," amesema Maguli.
Mshambuliaji huyo ambaye Jumapili iliyopita aliifungia timu ya taifa ya Tanzania bao la kusawazisha dhidi ya Benin, ukiwa ni mchezo wa kirafikia uliopo kwenye kalenda ya FIFA, amesema anataka kurudi Tanzania, kwasababu ligi yake inaushindani mkubwa ukilinganisha na ile ya Oman ambayo haina changamoto.
Maguli amesema malengo yake ni kucheza soka barani Ulaya, na anaamini akicheza Yanga ni rahisi kufikia malengo yake kwasababu ni timu ambayo inashiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara.
Kabla ya kwenda Oman, Maguli alianza kucheza soka la ushindani kwenye klabu ya Ruvu Shooting, na baadaye akasajiliwa na Simba ambako alidumu kwa msimu mmoja kabla ya kuvunja mkataba na kuondoka baada ya kocha wa wakati huo Dylan Kerr, kutoridhishwa na uwezo wake na mchezaji huyo alijiunga na Stand United ya Shinyanga aliyoichezea hadi alipopata dili la kwenda Oman.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment