MAKOCHA DIRISHA DOGO LINAWEZA KUWA MWOKOZI WA AJIRA ZENU



Nafasi ya mwisho kwa makocha wa timu za ligi kuu, katika kuhakikisha wanaboresha vikosi vyao ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu
Pazia la usajili mdogo, la msimu wa 2017/18 limefunguliwa jana Novemba 15, na litadumu hadi Desemba 15, kipindi hicho cha siku 30, kinatosha kwa klabu husika kufanya uhamisho wa wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao hasa kwa malengo waliyokuwa nayo.
Pazia hilo la usajili mdogo unahusisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Ligi Daraja la kwanza pamoja na ile ya daraja la pili ambazo zote zinasimamiwa na Bodi ya Ligi.
Katika idadi ya mechi tisa ambazo timu zote imeshazicheza niwazi makocha wote hasa wale wa Ligi Kuu, watakuwa wamebaini makosa yaliyopo kwenye vikosi vyao na kubaini mchezaji gani ambaye wanaweza kumsajili ili kuimarisha sehemu hiyo na mambo yakaenda sawa.
Hiki ndiyo kipindi ambacho makocha hasa wale waliokalia kuti kavu wanapaswa kukitumia vizuri kunusuru vibarua vyao kwani vinginevyo wanaweza kwenda na maji endapo dirisha litafungwa na wao kushindwa kusajili mchezaji yeyote na timu kuendelea kufanya vibaya.
Taratibu za usajili katika kipindi hiki zinaeleza kuwa timu inapaswa kusajili wachezaji ambao inahisi inaweza kuwasaidia katika mapungufu waliyokuwa nayo na siyo kutema mchezaji kwani huo siyo usajili wa dirisha kubwa la kipindi cha kiangazi.
Niwazi kuwa kila timu inamalengo ya kutwaa ubingwa na kila kocha angependa kuona timu yake inacheza vizuri na kutwaa ubingwa, hilo linawezekana endapo atakuwa na kikosi imara ambacho kinaundwa na wachezaji wazuri pamoja na mbinu bora kutoka kwake.
Mpaka kufikia sasa mzunguko wa tisa tayari tumeona baadhi ya makocha kadhaa wakitimuliwa kazi na wengine wakijiengua wenye kutokana na mwenendo mbaya wa timu husika hilo ni jambo la kiungwana kwasababu wamejipima kutokana na kile walichokitenda.
Kwa makocha waliobaki kwenye kazi, nivyema wakakitumia vyema kipindi hiki kurekebisha pale ambako waliona kuna mapungufu, timu kama Simba pamoja na kuwa na kikosi kipana na kuongoza ligi kwa sasa lakini imeonyesha mapungufu makubwa kwenye safu yake ya ushambuliaji.
Kocha Omog anapaswa kuukazia uongozi ili kusajili streka ambaye anaweza kumsaidia kumaliza tatizo hilo ili na yeye asiye kumfuata aliyekuwa msaidizi wake Jackson Mayanja ambaye aliamua kujiondoa mwenye tatizo kubwa likiwa ni mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Ikumbukwe kwamba Simba ni moja kati ya timu mbili zitakalo liwakilisha taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo nivyema ikajipanga kikamili ili iweze kufanya vizuri na kuepuka ile aibu ya timu za Tanzania kutolewa kwenye hatua za mwanzoni.
George Lwandamina huyo ni mmoja wa makocha ambaye kipindi hiki kitakuwa kinamuhusu kwa ajili ya kufanya usajili ambao unaweza kukiimarisha kikosi chake na kuweza kutetea ubingwa wake alioutwaa msimu uliopita lakini pia aweze kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo atashiriki.
Baada ya kuondokewa na wachezaji sita wa kikosi cha kwanza pamoja na kuwa na mwenendo mzuri lakini Yanga bado imeoneka na mapungudu makubwa katika idara zote na uongozi pamoja na kocha Lwandamina wanapaswa kushirikiana na kukifanyia kazi kipindi hiki cha siku 30, ili mambo yaweze kuwa sawa.
Zipo timu ambazo katika mechi 9 walizocheza hazijawapa matokeo mazuri na kujikuta zikiburuza mkia nazo kupitia kwa makocha wao zinapaswa kukitumia vyema kipindi hiki kufanya usajili ambao utabadili mwenendo wao na kufanya vizuri wakati ligi itakapokuwa inazidi kuendelea.
Kagera Sugar,  Maji Maji, Stand United na Njombe Mji ni timu ambazo zipo kwenye wakati mgumu na makocha wao kwa vipindi tofauti walikuwa wanakisubiri kwa hamu kipindi hiki kwa lengo la kufanya usajili sasa ndiyo wakati muafaka kwao cha kuweza kujinasua na janga la kupoteza kazi kwani kama utakuwa kimpya na dirisha kufungwa kisha timu ikaendelea kufanya vibaya tambua hakuna atakaye kufumbia macho hakuna kiongozi au shabiki anayefurah timu yake inapofungwa.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: