Ni baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nkwimbili wakiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa,Picha na Maiko Luoga Ludewa |
Na Salum Mhamed Ludewa,
Ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuchapa kazi kwa bidii wananchi wa kata ya lupingu wilayani ludewa katika mkoa wa njombe wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Shughuli mbalimbali za maendeleo zinazoendelea katika kaya yao.
Mh, Scander Mwinuka ni Diwani wa kata ya Lupingu wilayani Ludewa alisema kuwa jambo la kushiriki katika maendeleo ni jumuku la kila mwananchi kutokana na kasi ya serikali iliyopo madarakani inayomtaka kila mwananchi kuwajibika kwa nafasi yake ili kufikia Tanzania ya Viwanda.
Imeelezwa kuwa serikali pekeee haitoweza kumaliza changamoto zilizopo nchini bila wananchi kuonesha jitihada za kushiriki katika Shughuli za maendeleo zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali ya Nchi ikiwemo uchimbaji wa barabara,ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa shule na ujenzi wa nyumba za watumishi katika Kata ya Lupingu wilayani Ludewa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kidete wameipongeza halmashauri ya wilaya ya ludewa Ikiongozwa na mwenyekiti wa halmshauri hiyo MH Edwadi Haule pamoja na Mbunge wa jimbo la Ludewa MH Deo Ngalawa kwa kuwapelekea Mtambo aina ya Greda kubwa ambalo linawasaidia kuchimba barabara hiyo ambayo hapo awali walikuwa wakichimba barabara kwa kutumia zana za mikono.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment