TARULA YAPOKEA BARABARA 125 ZA HALMASHAURI YA WILAYA LUDEWA MKOA WA NJOMBE




 Na Salum Mhammed Ludewa,
 Halmashauli ya wilaya ya ludewa mkoani njombe imekabidhi  zaidi ya barabara 125 kwa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Tayari kwa kujengwa katika kipindi hiki cha msimu wa mwaka wa Fedha 2017\2018. 

Akizungumza na mwandishi wetu Meneja wa TARULA wilaya ya ludewa Eng.Butene Jilala Alisema kuwa kwa sasa wao kama Tarura wamejipanga kuanza ujenzi wa barabara ambazo zimekuwa hazipitiki wakati wa mvua kwakuzifanyia malekebisho barabara ambazo zilikuwa hazijakamilika zikiwa chini ya halmashauri hapo awali.

Alifafanua kwamba wilaya ya Ludewa ni kubwa hivyo wao watahakikisha wanaanza na barabara ambazo zilikuwa hazipitiki katika kipindi cha mvua ikiwamo barabara yakutoka Ludewa Mjini kuelekea katika Kijiji na Kata ya Ibumi pamoja na  barabara za kuelekea maeneo mengine ya Ludewa ambazo ni korofi hasa kwakipindi cha Masika.

Aidha alibanisha kuwa swara la ujenzi wa barabara wakati wa masika ni gumu hivyo aliwataka wananchi kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha masika ambacho TARULA imekabidhiwa barabara hizo kwani hivi karibuni mvua zitaanza kunyesha hivyo itakuwa ni vigumu kuzifanyia malekebisho barabara hizo wakati mvua zikiendelea kunyesha.


Katika hatua nyingine Meneja huyo wa TARULA wilaya ya Ludewa alimpongeza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh,Edward Haule kwakuendelea kushirikiana na wananchi wilayani Ludewa katika Kuhakikisha kuwa Barabara za vijijini zinaendelea kufunguliwa ili kuunganisha mawasiliano katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ludewa.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: