KWENDA DIRISHA DOGO, KOCHA AZAM FC AWALENGA WALIOPACHIKA MABAO


Keshokutwa Jumatano dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa, tayari nyota wawili wa Mbeya City na Prisons wamekuwa kipaumbele kwa Kocha wa Azam FC, Mromania, Aristica Cioaba.

Nyota hao ni Mohammed Rashid wa Prisons ambaye mpaka sasa ana mabao sita, pamoja na Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao manne. 

Wawili hao wameonekana wanaweza kutibu tatizo la ushambuliaji linaloisumbua timu hiyo.

Hivi karibuni, Azam iliachana na straika wake Mghana, Yahaya Mohammed, huku Aristica akitangaza kuingia sokoni na kuchukua mastraika wawili wazawa ambao anaamini watalitatua tatizo hilo linalowasumbua tangu kuanza kwa msimu huu.

Mmoja wa watu wa benchi la ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumatatu: “Majina ya Mohammed Rashid na Eliud Ambokile yamekuwa ya kwanza kutajwa na kocha kwani anadai amewafuatilia kwa umakini na kubaini kwamba wanamfaa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

“Kinachosubiriwa ni kamati ya usajili ikae iweze kuangalia uwezekano wa kuwasajili kutokana na mapendekezo hayo ya mwalimu.” 

Alipotafutwa Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, kuzungumzia masuala ya usajili ndani ya timu hiyo, alisema: “Baada ya mechi yetu ijayo ndiyo kamati itakaa kujadili ripoti ya kocha ili kuona nani anahitajika kusajiliwa kwa sababu kuna sehemu zinaonekana wazi kabisa bado zina upungufu.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: