ITAPENDEZA ZAIDI” YA DK SHIKA ISIINGIE USAJILI DIRISHA DOGO



KESHOKUTWA Jumatano dirisha dogo la usajili litafunguliwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya mechi 9, zitakuwa na nafasi ya kujipanga upya na kurekebisha sehemu am­bazo zinahitaji kufanya hivyo.

Baada ya mechi 9, timu zi­takuwa zimeona kulingana na zilipo. Nafasi zipi baada ya kukusanya kiasi kipi cha pointi na zenyewe zinajua ukusanyaji wake wa pointi ulipita katika njia zipi.

Wakati wa kufanya usajili wa maboresho ya kikosi, hak­ika unahitaji utulivu wa hali ya juu kwa ajili ya kuhakikisha safari iliyobaki inasomeka kwa mwendo sahihi baada ya ma­badiliko.

Kuangalia kikosi kilivyo, ma­bao ya kufunga na kufungwa yalikuwa mangapi. Ushindi na sare yanakuwa ni matokeo ya ujumlisho wa kilichofanyika hasa baada ya kuangalia ‘per­formance’ mfano, walinzi wali­cheza vipi, tatizo la kiungo na ushambulizi limekaaje.

Maana yake iko hivi, ili kupata majibu sahihi wakati wa dirisha dogo na dira ya nini cha kufanya. Benchi la ufundi linapaswa kupewa na­fasi kubwa zaidi ya kufanya uamuzi wa kipi cha kupunguza au kuongeza na isiwe viongozi wenye matakwa au kero zao ndiyo wageuke kuwa mako­cha.

Lengo hasa ni kutaka kuwa­kumbusha viongozi wa timu yoyote ile inayoshiriki Ligi Kuu Bara kwamba suala la dirisha dogo la usajili, zaidi linakuwa ni ‘mali’ ya benchi la ufundi kwa kuwa ndilo limeona kwa ukaribu zaidi kilichopun­gua na wana nafasi kubwa ya kujua mahitaji kwa maana ya kipi hasa kinachotakiwa kuongezwa.

Kama viongozi watachukua nafasi kubwa kwa kuwa wao ndiyo wanao waongoza ma­kocha na benchi la ufundi basi watakuwa hawatendi haki na ikiwezekana watakuwa wana­zuia kazi ya kiufundi ya mako­cha kufanyika katika misingi ambayo ni sahihi.

Lakini kama makocha nao watakuwa waoga, pia wa­takuwa wanaiangusha taa­luma yao kwa kuwa kama watapelekewa mchezaji wa­nayeamini hana msaada kwao na baadaye kweli akafeli, basi mwisho wao ndiyo watakaoan­guka na viongozi watakaa kan­do na kuwa sehemu ya wale wanaowasema wao kwamba wameshindwa.

Dirisha dogo, kazi yake ni kuimarisha. Hivyo huu ni wakati wa timu hizo kujiima­risha kupitia upungufu wali­opitia katika mechi tisa za Ligi Kuu Bara na halitakuwa jambo la mzaha kama alivyofanya Dk Louis Shika wakati alipok­wenda kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi zilipokuwa zinapigwa mnada.

Dk Shika alikubali kununua nyumba za Lugumi kwa zaidi ya Sh bilioni tatu akijua hana. Wakati mnada ukiendelea, al­isema “Nafikiri 900 itapen­deza zaidi.” Baada ya hapo msemo huo ndiyo umekuwa gumzo kila sehemu na hasa mitandaoni.
Faida ya msemo huo sasa ni utani na utaona, Dk Shika alikwenda kufanya mzaha ka­tika jambo ambalo wahusika hawakuwa wakihitaji utani za­idi ya kuhakikisha wanaifanya biashara kwa kuwa suala hilo halihusishi utani.

Ndiyo maana nawasisitiza viongozi kuwa, wakati wa diri­sha dogo la usajili, wanapaswa kuwa makini sana na utani wa Dk Shika kwa kuwa baada ya dirisha hilo, basi hakutakuwa nafasi ya mabadiliko hadi mwishoni mwa ligi.
Kama nafasi ndiyo hii, basi hakutakuwa na mzaha hata ki­dogo na vema mambo yakaen­da kitaalamu na kuangalia kile kilicho sahihi kwa kuwa haku­takuwa na nafasi nyingine tena ya kufanya marekebisho.

Matakwa binafsi, mihemko, kufanya mambo ili kupata bakshishi, lisiwe jambo litaka­lopewa kipaumbele badala yake umakini kwa njia za ki­taalamu ndiyo upewe nafasi ili kufanikisha kinachotakiwa kubadilishwa.

Nimeamua kuwakumbusha hivi kwa kuwa mara nyingi sana tumeona timu zikifanya mabadiliko wakati wa dirisha la usajili lakini baada ya diri­sha kufungwa na zenyewe kuwa zimefanya mabadiliko, mambo yanakuwa afadhali ya jana.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: