JULIO: TULIENI TU, MECHI ZA NYUMBANI ZITATUBEBA



Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
LICHA ya kufungwa mechi mbili mfululizo, Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameweka bayana kwamba ana uhakika mkubwa wa kucheza ligi kuu kwa msimu ujao kutokana na kubakisha michezo mitatu yenye pointi tisa wakiwa nyumbani.
Dodoma FC juzi Jumamosi walipoteza mchezo wao dhidi ya Biashara Mara kwa bao 1-0, wakiwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ambapo kwa matokeo hayo yameifanya timu hiyo kuporomoka kutoka kileleni hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 18.

Julio ameliambia Championi Jumatatu kuwa atahakikisha anakiandaa kikosi chake kufanya vizuri kwenye michezo hiyo ya nyumbani ili iweze kuibeba timu yake na kupata pointi ambazo zitawafanya watinge ligi kuu.

“Sina wasiwasi kwamba tunapata matokeo mabaya kwa sasa baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo, kikubwa tunaamini kwamba tuna nafasi kubwa ya kutinga ligi kuu msimu ujao, tumebakisha mechi tatu kwenye uwanja wetu wa nyumbani, kwenye michezo hiyo najua kabisa tuna uhakika wa kupata pointi zote ambazo zitafanya mahesabu yetu yakamilike,” alisema Julio




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: