Leo tena ZBC 2 kama kawaida wanakuletea mitanange ya Afcon kutoka Gabon. Hii leo wawakilishi pekee kutoka Africa Mashariki timu ya taifa ya Uganda The Cranes watatupa karata yao ya kwanza katika mashindano hayo zidi ya timu ya taifa ya Ghana.
Mechi hii inanikumbusha mwaka 1978 katika Afcon ya 7 iliyofanyika Ghana ambapo Ghana walikutana na Uganda na Ghana kuibuka kidedea kwa mabao mawili.
Ghana wanaonekana na hasira sana kwani kuanzia mwaka 2010 hadi sasa wameingia fainali ya AFCON mara mbili ikiwa ni 2010 na 2015 lakini zote hizo Black Stars waliibuka patupu. Safari hii wakiwa na Asamoah Gyan, Andre Ayew na Christian Atsu wanaingia kwenye mashindano haya kujaribu tena kulitafuta kombe hili.Na ni kati ya timu zinazotabiriwa kufanya vizuri AFCON.
Toka mwaka 1978 ambapo Uganda alifungwa na Ghana katika fainali za AFCON, The Cranes hawajawahi kushiriki tena AFCON hadi mwaka huu tena ndio wamerudi.Lakini Uganda chini ya kocha wao Micho hawataonekana kuwagopa Ghana kwani wameshacheza nao miezi mitatu iliyopita.
Ghana na Uganda walikutana katika mpambano wa kufuzu kombe la dunia huku The Cranes akiwalazimisha suluhu Ghana. Watakuwa wakijiamini zaidi huku langoni wakiwa na mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaochexa nyumbani Dennis Onyango.
Usikae mbali na remote yako kwani ZBC2 ndio mahala pekee kwa wewe mteja wa Azam Tv kuweza kujionea mtanange huu.Ghan kipigo kwa Uganda au Uganda atalipa kisasi? Angalia ZBC2.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment