AHUKUMIWA KIFUNGO MAISHA LUDEWA NJOMBE






MTU mmoja aitwaye Joel Lazina Ngailo, mwenye umri wa miaka 18 Mkazi wa Mlangali Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe, amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumwingilia kinyume cha maumbile mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi katika Mahakama ya wilaya ya Ludewa Mheshimiwa JOEL JOACHIM MWAKYOMO (JJ),mwendesha mashtaka wa polisi EZEKIEL MAGOSSO,akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 25 mwaka jana.
Akisoma hukumu hiyo Mheshimiwa Mwakyomo alisema kesi hiyo haina adhabu mbadala hivyo akamhukumu kutumikia kifungo cha maisha,kwa sababu upande wa mashtaka haujaacha shaka lolote juu ya mshtakiwa kuhusika na kosa hilo.
Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo, alisema haoni sababu ya kufanya hivyo kwa sababu hakutenda kosa hilo, akidai kuwa upande wa mashtaka umepandikiza ushahidi.hata hivyo yeye hakuleta mashahidi wa upande wake.
Wakati huohuo mtu mmoja aitwaye RAYMOND MWINUKA mwenye umri wa miaka 28 mkazi Madunda wilayani Ludewa amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kuchapwa viboko 12baada ya kupatikana na hatia katka kesi ya unyang;anyi wa kutumia silaha.
Akitoa hukumu hiyo jana hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Mh;JOEL JOACHIM MWAKYOMO(JJ),alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliopelekwa na upande wa mashtaka na kwamba hakuna shaka lolote.
AWALI mwendesha mashtaka wa polisi EZEKIEL MAGOSSO, aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda makosa yote matatu septemba 2 mwaka jana, ambapo baada ya kuwajeruhi kwa mapanga walalamikaji ASTELIA KAYOMBO na REHEMA MLELWA alifanikiwa kuiba jumla ya shilingi milioni 5,700,000.

SORCE.redio best fm ludewa

Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: