MAMA ALIYEPOTEA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA APATIKANA IBUMILA


NJOMBE

Kukosekana kwa Uzio katika Hospitali ya Kibena kumeendelea kusababisha baadhi ya wananchi kukosa imani na ulinzi na usalama wa hospitali hiyo  kutokana na wagonjwa kupotea wakati wakipatiwa huduma za matibabu.

Wananchi wa kutoka kata ya Mahongole wamesema serikali haina buni kuboresha mazingira ya ulinzi kwa wagonjwa wa hospitali ya Kibena ili wagonjwa wasiendelee kupotea kwani ndugu yao Maulisia Muhanze amepatikana huko Ibumila baada ya kupotea kwa siku nne wakati akipatiwa  matibabu hospitalini hapo.

Wamesema mama huyo Maulisia Muhanze alipotea Octoba 21 akiwa amelazwa katika hospitali ya kibena baada ya muuguzi wake kwenda kuandaa uji wa mgonjwa huyo na kukuta hayupo wodini hapo na kuendelea na juhudi za kumtafuta kwa siku nne bila mafanikio ambapo leo amefanikiwa kupatikana kijiji cha Ibumila.


Mama huyo Maulisia Muhanze amepatikana katika kijiji cha Ibumila baada ya matangazo ya kupotea kwa mama huyo kupitia radio Uplands fm ndipo wananchi wa kijiji hicho kumuona na kumpeleka kijijini kwao Mahongole.

Hivi karibuni Uplands Fm ilizungumza na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt Allen Kitalu alikili kuwepo kwa changamoto ya uzio huku baadhi ya viongozi akiwemo Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Edward Mwalongo Wakisema serikali inaendelea na jitihada za kufuta ufumbuzi wa tatizo hilo



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: