MKURUGENZI CHUO KIKUU HURIA ATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU KUJIANDAA NA MACHIMBO YA MIGODI YA LIGANGA NA MCHUCHUMA



MKURUGENZI WA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA TAWI LA  NJOMBE  DKT SUSAN GWALEMA AKITOA TAARIFA YA CHUO HICHO  KITUO CHA NJOMBE

NJOMBE

Serikali Mkoani Njombe Imetakiwa kushirikiana na wadau kuwaandaa vijana katika nyanja mbalimbali kuhusiana na shughuli zitakazoanza kufanyika kwenye machimbo ya migodi ya liganga na mchuchuma kwa kuanzia na matumizi ya lugha na shughuli za ujasiliamali.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa chuo kikuu huria Tawi la Njombe Dkt Suzana Gwalema wakati akizungumza kuhusiana na vijana kujiunga na chuo hicho ili  kuongeza taaluma na ujuzi  kwaajili ya maandalizi ya fursa zitakazokuwepo mara zoezi la machimbo ya migodi hiyo litakapoanza.

Dkt Gwalema amesema chuo kikuu huria tawi la Njombe kinaandaa mtaala wa ujasiliamali  kwaajili ya kufundishia vijana waliohitimu elimu ya sekondari ya kidato cha nne ambao utahusisha kozi ya tehama na kozi ya Utalii itakayokuwa na  lugha za kigeni ikiwemo ya kichina.


Katibu tawala msaidizi sehemu ya uzarishaji na Uchumi Mkoa wa Njombe Lameck Noa amesema serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kujiandaa na machimbo ya migodi ya liganga na mchuchuma kwaajili ya kupata fursa za masoko kutokana na ugenzi utakaokuwepo ambao utahitaji vyakula na mahitaji mengine muhimu .

Baadhi ya Wadau wa maendeleo Akiwemo padre wa kanisa katholiki jimbo la njombe meledius mlowe amesema maandalizi ya msingi ya mgodi yanatakiwa kufanyika kikamilifu kwa kuwalipa fidia wananchi wa eneo husika la machimbo huku vijana wakitakiwa kujipanga na uzarishaji mkubwa katika miradi hiyo.







Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: