Dar Es Salaam,Tanzania.
MSAFARA wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,unatarajiwa kuondoka jijini Dar Es Salaam, Jumanne Alfajiri ukiwa na kikosi cha nyota 20 na jopo la ufundi lenye watu 7 likiongozwa na Kocha Hans Van Pluijm kuelekea mkoani Mtwara tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho kutwa Jumatano dhidi ya wenyeji wao Ndanda FC.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na vuta nikuvute nyingi Yanga SC itawakosa nyota wake sita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na majukumu ya timu za taifa.
Nyota wataokaoukosa mchezo huo ambao ni wa pili kwa Yanga SC ni:
1. Deogratius Munishi ( Msibani )
2. Geofrey Mwashuiya ( majerhi )
3. Pato Ngonyani ( majeruhi )
4. Malimi Busungu ( majeruhi )
5. Haruna Niyonzima ( timu ya taifa )
6. Vicenti Bossou ( timu ya taifa )
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment