SIMU ZA MKONONI ZAATHILI MBEGU ZA KIUME


Tathmini ya utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini Uingereza, inaonyesha kuwa kiwango cha mbegu za uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko ya suruali.Hata hivyo ,mwanasayansi wa maswala ya uzazi na shahawa,anasema kuwa ushahidi huo bado hauna uhakika wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni mwake.Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la 'Environment International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki kuwa chanzo kikuu kinachoathiri mbegu za wanaume.Wataalamu walichanganua utafiti tofauti kuonyesha uborawa shahawa wakihusisha wanaume 1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika kliniki za uzazi.Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa kutokana na uchunguzi huo,mmoja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya utumizi wa simu na kudidimiakwa ubora wa shahawa."Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula."Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononiAlikubali kukosolewa na wanasayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na kuharibu"DNA" linatokana na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza changia kudidimia kwaubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote."Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya maisha."Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simuyangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruali yangu""



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: