ABAKA MWANAE WILAYANI LUDEWA


Tokeo la picha la MAHAKAMA LUDEWA


Mkazi mmoja wa kijiji na kata ya Mundindi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe anayefahamika kwa majina ya Batazari Mlowe mwenye umri wa miaka 47 mpangwa  sept,13,2016 amefikishwa katika mahakama ya wilaya Ludewa  akituhumiwa kwa kosa la kumuingilia kimapenzi mwanae ambaye jina lake limehifadhiwa ikiwa ni kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha 1 [a].

Akitoa taarifa hizo mtunza kumbukumbu msaidizi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Bw,Humbo Bornfast Nasson amesema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kulala na mwanae mnamo september 08 mwaka huu majira ya saa mbili usiku huko mundindi.

Aidha hatua ya kumpeleka mahabusu mtuhumiwa huyo ni kulingana na sheria ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kesi hiyo imesomwa kwa mara ya kwanza  september 13 mwaka huu na itatajwa kwa mara ya pili katika mahakama ya wilaya ya Ludewa september 28 mwaka huu.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: