Mshambuliaji wa Manchster United na Uingereza, Wayne Rooney ameandika historia ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu ya taifa ya England mara nyingi zaidi, kwa wachezaji wa ndani ya uwanja.
Ulikuwa mchezo wake wa 116 kuiwakilisha England alipocheza na Slovakia katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2018.
Rekodi hii inaipita ile ya David Beckham ambaye aliichezea timu ya Taifa la England mechi 115 huku Mlinda mlango Peter Shilton, ndiye anaishika rekodi ya jumla kwa kuichezea England mara 125.
Rooney ameweka rekodi hiyo kwa wachezaji wa ndani baada ya kucheza mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Slovakia ambapo Uingereza ilishinda 1-0 kwenye mechi hiyo.
Rooney anaweza kuifkia rekodi ya jumla ya Peter Shilton aliyecheza mara 125 akiwa kama kipa endapo mshabuliaji huyo atakuwa kwenye ubora wake.
Wiki iliyopita Rooney alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry anatarajia kuongoza mazungumzo na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov kwenye mkutano wa G20 ambapo watajaribu kuhitimisha mpango wa mapigano nchini Syria na kufungua misaada ya kibinadamu.
Umoja wa mataifa umekuwa ukishiriki kusitisha mapigano na kuruhusu misaada kwa jamii, licha ya kuwa na mazungumzo ya muda mrefu yamefanyika,lakini hakuna mpango wa makubaliano kufikiwa.
Waasi walio kwenye mkoa unayoshikiliwa wa Aleppo wanaripoti kuwa wapo chini ya ulinzi na wamezingirwa kwa mara nyingine baada ya vikosi vya serikali kukamata maeneo ya nje kidogo kusini Magharibi mwa wilaya ya Ramouseh siku ya jumapili.
Hatua hiyo inakuja baada ya pande hizo mbili kutofautiana katika masuala ya machafuko yanayondelea nchini Syria kwasasa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment