Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAADA ya safari ndefu ya saa kadhaa, kikosi cha Mbeya City FC tayari kimewasili jijini Mbeya kujiwinda na mchezo ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.
Meneja wa Mbeya City, Geoffrey Katepa amesema Mwalimu Kinnah Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni wataingia kwenye uwanja wa Sokoine kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo wa jumamosi.
Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake
“Mwalimu ametoa mapumziko siku ya leo hii ni kwa sababu tumekuwa na safari ndefu kutoka Mwanza tukipitia Tabora, hivyo mazoezi ya matayarisho ya mchezo ujao yataanza kesho jioni, jambo muhimu ni kwamba tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu mitatu ya mwanzo wa msimu,hili limetufanya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza, jambo ambalo pia limetuongezea morali kubwa ya kushinda dhidi ya Azam Fc jumamosi” alisema.
Akiendelea zaidi Meneja Katepa alisema kuwa kitengo cha utabibu cha City kinachoongozwa na Dr Joshua Kaseko kimesibitisha kuwa wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kwa maana ya hakuna aliye majeruhi na baada ya mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya kujiandaa kucheza mchezo wa jumamosi.
“Jopo la madaktari wetu wamenithibitishia kuwa kikosini hakuna mchezaji mwenye majeraha, wote wana hali nzuri hivyo baada ya kupisha mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya matayarisho ya mchezo”. alimaliza.
Kwenye michezo mitatu iliyopita City ilifanikuwa kuibuka na pointi 7, kufuatia suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto Africans bao 1-0 na mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc bao 4-1 na kushika usukuni wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment