Mo aweka mkwanja Simba ikiiua Azam



NA MWANDISHI WETU
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameongeza ‘mzuka’ wa wachezaji baada ya kutoa ofa ya bonus ya Sh milioni 10 ili waweze kucheza kufa kupona na kuibuka na ushindi dhidi ya Azam.
Simba wanatarajia kucheza na Azam kesho katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mo ameahidi kutoa Sh milioni 10 ambayo itaongezwa na milioni 10 nyingine ambazo hutolewa na wanachama kwa kujichangisha na kufanya bonus ifike Sh milioni 20.
Fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji ikiwa watashinda pambano hilo dhidi ya Azam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, lengo la kufanya hivyo ni kuongeza morali ya ushindi kwenye pambano hilo


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: