Karibu tulee… ni kondo la nyuma lakini, utaweza?
Kwa Blac Chyna, hicho ndicho amesema atakifanya.. kula kondo la nyuma (placenta) pindi akijifungua mtoto wake aliyempata na Rob Kardashian.
Model huyo mwenye miaka 28, ameuelezea mpango wake kwenye podcast ya Play.It’s Loveline with Amber Rose Jumatano hii. “Najisikia kuwa kwa mtoto wangu wa pili, nimeelimika zaidi kuliko wa kwanza,” Chyna alimweleza rafiki yake, Rose, 32.
“Ninasoma faida za kumnyonyesha mtoto wako, na hivi karibuni nimejifunza kuhusu vitu vipya, kuhusu kutokata kondo la uzazi. Kama umebaini, mbwa na paka, wanapozaa watoto wao, hula kondo la nyuma. Utasema hapa usifanye hivyo, lakini hufanya, na ni kitu cha afya,” alisisitiza.
Kula kondo la nyuma si kitu kigeni hata hivyo katika nchi mbalimbali. Kondo la nyuma ni ogani inayojishikilia katika ukuta wa nyumba ya uzazi ambayo huunganika na kitovu cha mama na hivyo huwa kama daraja linalomuunganisha mama na mtoto kabla hajazaliwa.
Hufanya kazi ya kusafisha hewa safi, damu, huchuja chakula na kukitoa kwa mama kwenda kwa mtoto na kazi zingine. Baada ya mama kujifunza, hutupwa na huwa halina kazi tena. Lakini wengine hulichukua na kulikaanga na kula kama nyama na wengine hulikausha na kutengeneza vidonge na pia wapo wanaolila likiwa bichi hivyo hivyo mara tu baada ya kutoka tumboni kwa mama.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment