KITUO cha Mabasi cha Songea mjini kinatarajiwa kufunguliwa Septemba 7 mwaka huu . katika kikao cha wadau wa usafirishaji ambacho kimefanyika leo na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Mahenge,wadau hao wa usafirishaji wamepitisha kwa pamoja kuwa Stendi ya Songea mjini itatumika kwa ajili ya daladala zote ambapo kituo cha Mabasi cha Msamala kitatumika kwa ajili ya Mabasi yote yanayosafiri nje ya Mkoa wa Ruvuma na yanayosafiri ndani ya Mkoa wa Ruvuma. Stendi ya Mabasi ya Songea mjini in a uwezo wa kukaa Mabasi 96 na daladala 29 ambapo Stendi ya Mabasi ya Msamala in uwezo wa kukaa Mabasi 112 ,daladala 212 na Mabasi mdogo 84.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemwagiza Mkurugenzi wa manispaa ya Songea kuanzia Septemba 7 kuanza kutoza ushuru katika Mabasi, daladala,taksi na toroli katika stendi ya Songea mjini.Tayari kitengo cha TEHAMA kimeshaingiza kwenye mfumo viwango vya tozo vitakavyotumika ambapo Mabasi ya Mkoa sh.3000,Mabasi ya wilaya sh.2000,daladala sh.1000,taksi ndani ya Stendi sh.3000, gari ndogo binafsi sh.500 na toroli sh.500
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment