DAR: CHADEMA yatangaza kuhairisha ‘Operesheni UKUTA’ hadi Oktoba Mosi


Habari wakuu,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, dakika chache zijazo kuna mkutano wa waandishi wa habari makao makuu ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA). Tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.
========
MBOWE
Amaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa na anaongelea uamuzi wa jeshi la wananchi kufanya usafi na urushaji wa ndege siku ya leo ambayo anasema haijawahi kufanya tangu uhuru.
Anasema anavyozungumza, katibu mkuu(Salum Mwalimu) anaendelea kushikiliwa na polisi mji wa Bariadi na ilikuwa leo apelekwe mahakamani lakini polisi wamesema wako bize.
Freeman Mbowe amesema maandamano ya UKUTA yameahirishwa kwa mwezi mmoja hadi tarehe Oktoba Mosi.
Mbowe: Tumepata wakati mgumu kufikia uamuzi, sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu. Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni. Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.
Mbowe: Ni matumaini yangu wana CHADEMA watatuelewa kamati kuu, asanteni sana kwa kunisikiliza.
Kinachoendelea kwa sasa ni maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
Kwa nini hamjapeleka shauri mahakamani: Mbowe: Yamepelekwa mashauri mengi mahakamani na yataendelea kupelekwa. Hatuwezi kuwalazimisha mahakama, hata kipindi hiki kuna mashinikizo kwa baadhi ya mahakama watoe maamuzi watoe maamuzi yanayorandana na serikali, wapo waliosimamia sheria lakini mahakimu nao ni binadamu.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho watu wawe barabarani, wanachama wetu ambao watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata Lowassa amaengea na mama Maria Nyerere wametusihi.
Mbowe: Viongozi waliomba wiki mbili mpaka tatu lakini sisi tukasema hapana kuna wengine tutakuwa na majukumu bungeni na hili jambo ni la kitaifa. Hatuna nia ya kuchafua Taifa, tuna nia ya kusaidia Taifa.
Mbowe: Mpaka jana tulikuwa na viongozi 230 amabao wameshtakiwa, viongozi 28 mapaka jana walikuwa hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu zetu akiwemo naibu katibu mkuu Zanzibar.
Mbowe: Nisikitike siku za karibu mahasimu wetu wamekuwa wakijaribu kutugombanisha ndani ya CHADEMA, hizi fitna za mitandao. Mbowe sina tabia ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama, Tamko nililotoa ni la leo.
Lowassa: Mitandao inaandika mambo mengi sana ambayo ni just accusations, ningekua na muda ningefafanua



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: