Yaliyojiri katika mechi ya kirafiki baina ya timu ya watangazji wa kituo cha redio best family na timu ya kijiji cha madindo fc kutoka kata ya ludewa.
|
katikati ni katibu wa mbunge wa jimbo la ludewa Ndg.Fungatwende kushoto ni timu kapteni wa Best family salum mohamed a.k.a fundi kulia ni meneja mkuu wa redio best fm ludewa wakiteta jambo kabla ya mechi
|
|
mashabiki wa timu ya madindo fc wakishangilia ushindi wao
|
|
katibu wa mbunge akisalimiana na wachezaji wa best family ya ludewa
|
|
katibu akisalimiana na timu ya madindo fc
|
|
Mtangazaji wa kituo cha redio best fm ludewa Nicksoni mahundi pamoja na meneja mkuu wa best fm mshairi wakimkaribisha mgei rasmi ambaye ni katibu wa mbunge wa jimbo la ludewa Ndug fungatwende |
|
picha ya pamoja ya vikosi vya mpira wa miguu best family na mdindo fc
|
|
katibu wa mbunge akitoa zawadi ya jezi kwa timu ya madindo fc
Katika harakati za kukuza michezo mbalimbali katika wilaya ya ludewa uongozi wa Radio Best fm Ludewa kupitia katika kipindi cha best sport kinacholuka kila siku kuanzia sa 2 kamili hadi saa 3 kamili usiku kwa pamoja wameunda kikosi cha mpira wa miguu ambacho kinacheza mechi mbalimbali za ndani na nje ya wilaya ya Ludewa ambao unakwenda kwa jina la msimu wa amsha amsha michezo 2016. juma pili hii timu hiyo ya watangazaji wa radio best fm ilishuka dimbani kucheza na timu ya kutoka katika kata ya ludende kijiji cha madindo. mchezo huo ulikuwa mzuri na wakuvutia mashabiki walio furika katika uwanja wa halmshauli ya wilaya ya Ludewa hadi dakika tisini zinamalizika best family walikuwa wamechapwa magoli mawaili wa moja. katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa ni katibu wa mbunge jimbo la Ludewa Ndg.Fungatwende aliyetumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kupenda michezo ili kuepukana na vitendo viovu. pia ndug Fungatwende licha kuwapongeza madindo fc kwa mchezo mzuri na wenye Nidhamu na kutoka na ushindi katika mechi hiyo dhidi ya best family alioa zawadi ya jezi set moja kwa timu ya madindo fc. lakin hakuwa mbali kukisifu chomba cha habari cha redio best fm ludewa kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza michezo na kuendeleza michezo mbalimbali katika wilaya ya Ludewa ikumbukwe ni msimu wa Amsha Amsha 2016 redio Best fm Ludewa inazunguka katika vijiji mbalimbali ili kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali katika wilaya ya ludewa
2016 tupo karibu yako
|
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment