MABINGWA wa UEFA CHAMPIONZ LIGI Real Madrid Leo wanakutana na Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI Sevilla huko Lerkendal Stadium Nchini Norway kugombea UEFA SUPER CUP.
Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Timu za Spain pekee kugombea Kombe hili ambalo huashiria kuanza kwa Msimu mpya wa Ulaya wa Mashindano ya Klabu ya UEFA.
Real wanatinga kwenye Mechi hii bila ya Mastaa wao Toni Kroos, Gareth Bale, Pepe na Cristiano Ronaldo wakati wengine kama Luka Modric, Sergio Ramos, James Rodríguez na Karim Benzema, ndio kwanza wamerejea Kikosini baada ya kutoka Vakesheni.
Lakini hilo halimbabaishi Kocha wa Real Zinedine Zidane kwa kuyakosa majina makubwa na amesema watafanya kila wawezalo kutwaa Taji lao la kwanza la Msimu mpya wa 2016/17.
Hii itafanya Real iwatumie Lucas Vázquez, James Rodríguez na Álvaro Morata huko mbele huku Casemiro, Luka Modric na Isco wakicheza Kiungo wakati Ramos, ikiwa Zidane atamwona yuko fiti, akianza Difensi pamoja Varane, Carvajal na Marcelo.
Kipa anatarajiwa kuwa Kiko Casilla badala ya Navas ambae anauguza Mguu wake.
Kwa upande wa Sevilla, ni wazi ni Timu tofauti kwa sasa toka ile iliyotwaa UEFA EUROPA LIGI Mwezi Mei kwani sasa wana Kocha Mpya kutoka Argentina Jorge Sampaoli baada ya yule Kocha mchawi wao Unai Emery kuhamia Paris Saint-Germain pamoja na Sentahafu Grzegorz Krychowiak.
Wengine walioondoka Sevilla ni Kevin Gameiro alienda Atlético de Madrid na Ever Banega kutua Inter Milan.
Hao Wanne walikuwa ndio Mioyo na Roho ya Sevilla.
Lakini nae Kocha mpya Jorge Sampaoli amekuja na wapya Kranevitter, Sarabia na Vietto
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment