MAMBO 10 YANAYOWACHUKIZA WANAUME.
Wanawake wengi huamini kuwa uzuri wa maumbile ni jambo la muhimu sana kwa mwanaume jambo ambalo sio la msingi kabisa katika kujenga penzi linalodumu.Uzuri wa maumbile unaweza kumvuta mwanaume kuanzisha uhusiano lakini sio kitu ambacho kinaweza kuwa nguzo muhimu ya kudumisha uhusiano huo. Mwanaume anahitaji mwanamke ambae atakuwa chemchemu ya kudumu ya furaha katika maisha yake. Yafuatayo ni mambo kumi ambayo hunyausha penzi la mwanaume.
1. Kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi (SMS) mara kwa mara na kulaumu pale ambapo mwanaume hapigi simu mara kwa mara au kutuma SMS. Siku hizi kuna SMS zilizotungwa ambazo zina maneno mazuri mazuri ya kimashairi na wanawake wavivu huzitumia hizo kuwatumia wanaume kuonyesha mapenzi yao, ukweli mara nyingi zinakuwa kero kwa wanaume kwa kuwa hazina uhalisia unaotoka kwa mtumaji. Wanawake wenye tabia hii hawajui umuhimu wa kumfanya mwanaume akumiss kwa muda fulani. Iwapo sitaki kukushirikisha ninavyoweza swali lako litanifanya nijisikie vibaya kwako nachukia kusema uongo hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka kunilazimisha kukueleza kila kitu kilicho moyoni mwangu.
2. KUKUBALIANA NA KILA KITU
Mwanamke ambaye anaogopa kuachwa, kufokewa na yuko tayari kufanya jambo lolote lile ili kumfurahisha mwanaume anaboa. Sio hilo tu bali inaumiza kuona kuwa umekuwa mpokeaji zaidi ya mtoaji na hali hii huzalisha uchungu na dharau ambayo haimsaidii mwanamke. Upo umuhimu wa mwanamke kuonyesha kuw nayeye ana mawazo mazuri kwa kukataa kukubaliana na kila kitu anachosema mwanaume.
3. KUTAKA KUJUA MAWAZO YA MWANAUME
Mwanaume anapokaa kimya sio kwamba amekasirika bali anapanga mambo yake na hataki kuingiliwa. Wanawake wengi waonapo mwanaume yuko kimya hukimbilia kuuliza “unawaza nini?” swali hili ni kero mbaya sana kwani unaingilia uhuru wa mtu mwingine. Tatizo hili linaenda pamoja na mwanamke mwenye tabia ya kutaka kwenda na mumewe kila mahali. Hali hii sisi wanaume tunachukia sana. Iwapo sitaki kukushirikisha ninavyowaza moyoni mwangu, swali lako litanifanya nijisikie vibaya kwani nachukia kusema uongo hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka kunilazimisha kukueleza kila kitu kilicho moyoni mwangu.
4. WASIOJISHUGHULISHA VYA KUTOSHA KITANDANI
Mchezo siku zote huhusisha pande mbili na katika tendo la ndoa ni hivyo hivyo. Asilimia 85 ya wanawake ni wavivu katika tendo la ndoa jambo ambalo ni kero kwa wanaume. Kwa kuwa wanaume wana tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kumaliza mwanamke ambaye hajishughulishi wakati wa tendo la ndoa huzalisha hasira kwa mwanaume. Mwanaume afanyapo tendo la ndoa kwa ufanisi mzuri hasa akirudia zaidi ya mara moja anakuwa amepunguza makali ya kichocheo (hormone) cha TESTOSTERONE, kichocheo hicho kikipungua na hasira hupungua. Kutokana na ukweli huo uvivu wa mwanamke kitandani mara nyingi humkasirisha mwanaume. Kwa kuwa mwanaume huyo hawezi kumwambia mwanamke mapungufu hayo hasira hiyo hujitokeza katika maeneo mengine tofauti kabisa jambo ambalo huwashangaza wanawake wengi.
5. KUTUMIA TENDO LA NDOA KAMA SILAHA
Wanaume wote hupendelea tendo la ndoa hadi katika Biblia ikaandikwa “MSINYIMANE” (2 KORINTHO 7) wanawake kwa kufahamu udhaifu huu wa wanaume wamewanyima wanaume unyumba kwa manufaa yao na kutumia tendo la ndoa kama adhabu au njia ya kulazimisha mabadiliko upande wa mwanaume.Mtazamo na tabia hii hubomoa nyumba.
6. WACHAFU
Hakuna mtu ambae anafurahi kuwa karibu na mtu anaetoa harufu mbaya. Wanawake wengine hujisahau na hawana tabia ya kupiga mswaki wakati wa kulala na inapotokea saa tisa usiku mwanaume anataka tendo la ndoa harufu mbaya toka mdomoni inamkasirisha mwanaume japo hatalalamika au kusema lolote. Mwanamke asipotumia maji kujiosha baada ya haja kubwa apanuapo miguu harufu ya choo ni chukizo kubwa. Kutojiosha baada ya raundi ya kwanza ya tendo la ndoa husababisha uume uteleze kupita kiasi na wanaume wengine huishia kutafsiri kuwa mwanamke huyo ana uke mpana jambo ambalo linawatuma wanaume kufukuzia mabinti wadogo au kuomba mchezo kinyume na maumbile. Mara nyingi mwanaume alie naye hatasema juu ya udhaifu huu na utashangaa tu kuona penzi limeshuka na kuendelea kunyauka.
7. VING’ANG’ANIZI
Wanaume wengi huchukia wanawake ambao hupenda kuwang’ang’ania kiasi ambacho wanajiona kama wamekuwa mateka au wafungwa gerezani. Wanawake ving’ang’anizi ni wale ambao hawajiamini na wanaogopa kuachwa au kusalitiwa kila dakika .Pale ambapo mwanamke anajaribu kumchunga mwanaume kwa kupiga simu mara kwa mara au kuuliza maswali yasio na msingi. Maswali kama upo wapi, uko na nani? Ulikuwa unaongea na nani kwenye simu? N.k ni kero kubwa sana kwa mwanaume. Inakuwa ngumu sana kumfurahisha mtu ambaye muda wote anajiona yuko katika hatari ya kuibiwa, anakuwa hana amani pale mwenziwe awapo mbali. Hali hii inawachosha sana wanaume na kutamani kujificha zaidi na zaidi jambo ambalo linamtesa mwanamke alie king’ang’anizi.
8. WAKANDAMIZAJI HOJA
Wakandamizaji wa hoja nI wale ambao hupenda kumkumbusha mpenzi wake jambo ambalo tayari alishamwambia mara kadhaa na mwenzie hajalifanya bado. Mwanamke hufanya hivi bila kujua kuwa ni jambo la hatari sana. Hali hii huwa kama sumu pale inapokuwa ina husu udhaifu au makosa fulani kwa kuwa hakuna anaefurahia kukosolewa mara kwa mara. Kumuuliza mwanaume mara kwa mara kwanini hakufanya jambo fulani hutafsiriwa kama dharau na hilo laweza kugeuka kuwa sumu kama sauti ya ukali inatumika. Kumwambia mwanaume afanye jambo ambalo hayuko tayari kulifanya.Ukandamizaji wa aina hii unanyausha penz taratibu sana. Kwa mfano kuuliza lini atakutambulisha kwa wazazi au ndugu zake,lini anapamga mfunge ndoa au lini mtatembelea wazazi wako na kadhalika. Kukandamiza hoja mara nyingi kwa mwanaume huonekana kama dharau. Asilimia 96% ya wanaume waliohojiwa wanasema kuwa mwanamke anakuwa mkandamizaji wa hoja pale anapotaka mwanaume afanye jambo fulani ambalo tayari mwanaume anajua anatakiwa kufanya hivyo na hilo kwa wanaume ni usumbufu mbaya. Utafiti uliofanywa na DR. HOWARD MARKHAM wa kituo cha Marital and family huko DENVER MAREKANI unaonyesha kuwa ukandamizaji wa hoja una nguvu sawa na uzinzi katika uvunjaji wa ndoa. Mwanamke anayeamini kuwa asiporudia kumwambia mumewe jambo fulani mumewe hatafanya na marudia hayo yatamfanya mwanaume ajione kama mtoto na huzaa chuki.
9. WIVU MCHAFU
Wivu huonekana pale ambapo mwanamke anahofu kuwa huenda mpenzi wake ataanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine hasa iwapo mwanamke mwingine mzuri kuliko yeye anakuwa karibu yake. Wivu unakuwa mchafu pale ambapo hakuna sababu dhahiri ya mwanamke kumshuku mumewe. Mwanamke wa aina hiyo anafanya kama vile mwanaume ni mali yake. Utakuta mwanaume anaulizwa maswali mengi mno kama vile yupo Kituo cha polisi Nyendo za mwanaume kufuatiliwa kwa karibu sana na mara nyingine hufikia kukatazwa kuwa karibu na watu au marafiki fulani. Mara nyingi mwanamke huyo akiambiwa kuwa ana wivu hukana na kuhalalisha tabia zake kwa visingizio mbalimbali. Hayo yote ni machukizo makubwa kwa mwanaume.
10. WAONGEAJI KUPITA KIASI
Ni kweli kuwa wanawake wameumbwa kuwa waongeaji na ndio maana tafiti zinaonyesha kuwa wanawake ni wepesi zaidi wa kujifunza lugha mpya kuliko wanaume. Katika sayansi ya mapenzi inakadiriwa kuwa mwanamke anaweza kuongea maneno 20,000 kwa siku wakati mwanaume uwezo wake unakadiriwa kuwa na maneno 7,000 tu kwa siku. Mwanamke aongeae kupita kiasi mara nyingi anakuwa hajijui kuwa ni tatizo kwani yeye mwenyewe anajiona kuwa kama mtoa burudani mzuri kumbe bila kujua anawaboa wengine. Mara nyingi mwanaume anapata shida kumkatisha na mara nyingine anaogopa kumkatisha ili asije akamkasirisha mpenzi wake. Kwa kuwa mwanamke huyo ni muongeaji sana utakuta mpenzi wake tayari anajua mambo mengi ambayo mwanamke huyo hupenda kuongelea na pia anajua mitazamo yake juu ya mada mbalimbali hivyo urefu wa maongezi yake mara nyingi inakuwa kero iletayo chuki. Muongeaji huyu wa kike tayari atakuwa anafahamika kwa marafiki wa mwanaume huyo na hivyo marafiki wa mume watakuwa wanamkwepa rafiki yao pale wanapojua atakuwa na mke wake (au mpenzi wake), hilo ni pigo kwa mwanaume. Marafiki hao watamwogopa mwanaume huyo kwani wanajua akiwepo mkewe basi bomba la mazungumzo marefu litang’oa masikio yao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment