Madrid,Hispania.
WAKATI kinyang'anyiro cha kumpata mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya kikitarajiwa kufanyika leo,mmoja kati ya wanaoiwania tuzo hiyo,Mreno Cristiano Ronaldo,ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake wa karibu AntoineGriezmann siyo kwamba hastahili tuzo hiyo bali pia hakustahili kuwa mchezaji bora wa michuano ya Euro 2016.
Kauli hiyo ya Ronaldo imetafsiriwa kuwa ni kijembe na jibu kwa Griezmann ambaye mapema wiki hii alidai kuwa yeye ndiye mwenye sifa za kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya mbele ya Cristian Ronaldo na Gareth Bale.
Pepe
Ronaldo amesema tuzo hiyo alistahili apewe Mreno mwenzie Képler Laveran Lima Ferreira maarufu kama Pepe na siyo Griezmann.
Akifanya mahojiano na mtandao wa UEFA.com,kupitia Goal,Ronaldo amesema "Katika kitabu changu,Pepe alikuwa bora sana msimu huu.Bila shaka alikuwa mchezaji bora katika kikosi cha Ureno na mmoja kati ya wachezaji bora wa Real Madrid katika michuano ya ligi ya mabingwa.
"Nimefurahi kuona akichaguliwa katika kikosi cha wachezaji bora wa Euro,kwa maoni yangu Pepe alistahili kuwa mchezaji bora wa Euro 2016.
Griezmann alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Euro 2016 baada ya kuifikisha Ufaransa katika hatua ya fainali akipachika mabao sita na kupika (assist) mengine mawili.
Griezmann,Ronaldo na Bale watakutana tena leo katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa Ulaya huko Monaco Ufaransa ambako pia droo ya upangaji wa makundi cha michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na ile ya Europa Ligi itafanyika.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment