Na Isack Makundi, Babati-Manyara
Napenda kumshukuru Mungu kwa wema wake mkubwa kwa amani ambayo ameendelea kutupa Tanzania wengine wanaitamani lakini hawaipati.
Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa Yanga chini ya billionaire Yusuph Manji kwa hatua waliofikia kwenye michuano ya CUF. Pia natoa lawama kwa wachezaji wa Yanga kwa kutotimiza wajibu wao kwenye michuano ya CUF huku wakitimiziwa kila kitu na uongozi na kubaki na hadithi za kizamani kuwa hawana bahati wakumbuke kuwa kwenye soka bahati ni 0.01%, jambo lolote ni kujituma hakuna zaidi ya hapo. (heko kwa D. Ngoma, Simoni Msuva wanajituma sana).
Pia nawashukuru sana wasomaji wa makala zangu kwa kunilazimisha kutoa maoni yangu kuhusiana na sakata la Yanga kukodishwa na billionaire Yusuph Manji wengi walinipigia simu, kutuma sms wakiuliza maoni yangu kama mdau wa michezo.
Ndugu zangu Waislamu mtanisaheme mimi napenda kunukuu maandiko kutoka kwenye biblia hii ni kutokana na imani yangu lakini nawapenda/nawaheshimu sana Waislamu, watanzania tuna dini lakini hatuna udini wote tunamwabudu Mungu mmoja.
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 2:18-25 utaona ni jinsi gani Mungu baada ya kumuumba Adam akamfanyia msaidizi wake kwa maana aliona huyu ni binadamu hajakamilika 100% lazima kuwepo na mtu wa kumshauri. Ndiyo maana Mungu anawataka wanadamu kutubu dhambi maana anajua wanadamu tunamapungufu mengi sana.
Nimeona nianze na utangulizi huo kwa sababu siku moja nikiwa form I mwaka 2001 nilitamani kusoma shule moja Arusha lakini kutokana na gharama zake kuwa kubwa mama yangu alikataa kunipeleka kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, kwa hasira nilimuuliza mama kwa nini sisi kwetu ni maskini naye kwa hasira akanijibu kuwa muulize baba yako.
Sikujua anamaanisha nini ni muulize baba yangu, baada ya kuwa mtu mzima ndiyo nimepata jibu kuwa kumbe baba ni kiongozi wa familia lakini baba yangu alikuwa hashauriki anajua kila kitu kama vile ni malaika. Viongozi wengi wa Afrika hawashauriki ndiyo maana nchi zetu ni maskini maana hawataki mawazo mbadala wao ni Alfa na Omega lakini Mungu aliweka washauri hakukosea.
Nawapongeza viongozi na wanachama wa Yanga kwa kufikia maamuzi ya kidemokrasia ya kuikodisha timu yao. Kama kuna mtu hatambui mchango chanya wa billionaire Yusuph Manji ndani ya Yanga basi huyo atakuwa na matatizo. Billionaire Yusuph Manji ni binadamu ana mazuri mengi anamafanikio makubwa sana kibiashara hata mimi nayatamani kila siku namuomba Mungu lakini inabaki kuwa ni uamuzi wa Mungu kama atanipa ama la sijui. Pia billionaire Yusuph Manji anaipenda Yanga kwa moyo wake wote, lakini billionaire Yusuph Manji ni binadamu anamapungufu yake.
Wazo la kuikodisha Yanga siungi mkono hata kidogo kwa sababu ambazo nitazitaja hapa chini kulingana na uelewa wangu mdogo.
- Makao makuu/Ofisi ya Yanga yatakuwa/itakuwa wapi?
- Timu ya vijana itawa chini ya nani?
- Yanga ni Sports Club je, ikianzishwa timu ya netball na yenyewe itachukuliwa?
- Kutakuwa na uchanguzi tena ama ndiyo basi tena?
- Billionaire Yusuph Manji ataendelea kuwa Mwenyekiti?
- Kwa nini 75% na siyo chini?
- Billionaire Yusuph Manji amekuwa kiongozi tangu 2012 kwa nini wazo hili limekuja ghafla hivi?
- Yanga ni taasisi inawatu wengi wanachama na mashabiki kwa nini kusiwe na muda wa kutosha kujadili jambo hili kwa mapana na marefu?
- Lini utafiti umefanyika kuona faida na hasara za kukodisha timu?
- Wanachama ni Dar es Salaam pekee mikoani hakuna?
- Kwa nini jambo hili jema liwe la dharura?
- Yanga ina wanachama wagapi nchi nzima na wangapi wameafiki jambo hili?
- Kwa nini kusiwe na grace period hata ya miaka miaka 3 kwanza?
- Je ikitokea timu ikashuka daraja au yenyewe ni milele haiwezi kushuka daraja nani atawajibika?
- Kwa nini isitangazwe kuwe na ushindani lakini Manji akapewa kipaumbele?
- Madeni ya timu yametokana na nini?
Haya ni baadhi ya maswali machache ambayo nimejiuliza sana baada ya kusikia ukondishwaji wa Yanga. Nimesikitika sana kusikia mtu anasema wanachama hawana msaada kwa timu sikutegemea kauli hiyo kutolewa na kiongozi msomi kama huyo.
Niwe mkweli tatizo la Yanga ni uongozi na siyo wanachama hawana msaada mbali ni viongozi kukosa ubunifu ama ni waoga(Hosea 4.6), haiwezekani leo hii mtu anatoa shilingi elfu 12 kwa mwaka anakuwa na sauti ndani ya timu, pia mawazo ya kumtengemea mtu mmoja kila anachosema ndiyooooo, kwa nini msihoji kwa mapana na marefu? Yanga ni taasisi haiwezekani jambo kubwa kama hilo likaletwa kwa dharura ndani ya saa 2 limejadiliwa na kupitishwa.
Madeni mengine Yanga inayatengeneza yenyewe bila sababu mfano timu kuruhusu mashabiki kuingia bure, kununua wachezaji kwa bei kubwa huku hawana msaada kwenye timu, timu kukaa Uturuki kwa nini isikae Zanzibar au Lushoto?
Tatizo Afrika hatuamini maskini kuwa anaweza kuwa na mawazo chanya tunaamini tajiri ana mawazo chanya pekee ndiyo maana akawa tajiri kitu ambacho ni wrong kabisa. Matajiri wengi mali ni za urithi kutoka kwa wazazi na hilo lipo wazi siyo wote wameanzia chini japo kuna wengine walianzia chini lakini ni wachache sana.
Mimi siwezi kuzuia wanachama kukodisha timu yao ila napinga utaratibu uliotumika, leo hii sawa unaachiwa majengo, haya majengo ni ya mwaka 1970 enzi ya marehemu Karume, baada ya miaka 10 ijayo si yatakuwa magofu na nani atayakarabati?
Pia nimesikitishwa sana na uongozi wa Yanga pamoja na wanachama wao huu utaratibu wao wakufukuza viongozi kama wanyama kwenye mkutano mkuu, wameitwa saa ngapi kujieleza? Kwa nini Jerry Muro analalamika hakuitwa na TFF kujieleza na wakati wao wanamfukuza kiongozi mbele ya mkutano mkuu na wanachama kuanza kumzomea (Hashim Abdallah) ambaye alikuwa amekaa meza kuu (Habari leo la 7.8.16) ni tabia isiyofaa lazima niiseme, chukulia kama billionaire Yusuph Manji angefanyiwa hivyo au Jerry Muro? Club yenye wasomi wazuri inafanya mambo ya aibu kama hayo inenisikitisha sana, watu wanaogopa kuuliza maswali sababu ya mambo ya kitoto kama haya ambayo ni aibu kwa taifa.
Mtu anafamilia yake anaonekana kwenye TV anafukuzwa/anazomewa kama panya, akianguka na BP akafa? Familia yake itatunzwa na nani? Hata kama anamakosa binadamu anahadhi yake, kuna mwingine unaweza kumsabishia stroke/pooza, wanachama acheni hivyo mtu kuwa maskini siyo tiketi ya kudhalilishwa/kuzomewa.
Inavyoonekana Yanga hakuna vikao vya ndani kama viongozi mkajadiliana? Mtu akikosa mara moja ni kufuza tu hakuna namna, siku akikosa billionaire Yusuph Manji na yeye atafukuzwa mbele ya mkutano mkuu?
Yanga imekuwepo toka 1935 viongozi wangapi wamepita pale? Wote mtapita lakini Yanga itaendelea kuwepo. Fanyeni mambo kama watu ambao wameelimika, ndiyo faida ya kuitwa msomi siyo kila jambo ndiyoooo, huyu ni binadama hawezi kuwepo milele atapita hana mkataba na Mungu.
Tatizo viongozi wengi Afrika hawataki kushauriwa/kukosolewa wala mawazo mapya yaani wao ni malaika, penye watu wawili au watatu lazima kuwe na kiongozi hatuwezi wote kuwa viongozi au matajiri. Kwa tabia hizi Afrika haitakaa iendelee sababu viongozi wengi ndiyo hawa tulionao. Majadiliano/kupingana kwa hoja ni njia sahihi ya kufikia mwelekeo mzuri.
Hitimisho
Kaeni mtafakari uamuzi wenu msikurupuke mtakuja kupata laana ya waanzilishi wa timu ambao pamoja na umaskini wao waliweza kufanya mambo makubwa jampo hawakuwa wasomi lakini walikuwa na maono/elimu zaidi ya hawa wasomi tulionao.
Andikeni andiko liwasilishwe kwa wanachama na watu wachambue faida na hasara za kukodisha timu.
Tunapokosoa tunakusoa kwa nia ya kujenga na hakuna mtu mbaya kama anayekubali kila kitu bila kuhoji.
Nimeandika kama shabiki wa Yanga na sina mchango wowote ndani ya Yanga zaidi ya kuwa mdau wa michezo na kwa yale mapungufu mtanisamehe mimi siyo malaika haya ni mawazo yangu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Yanga.
Ujumbe wangu wa leo Yer: 17.5
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment