1. Ni nyota wa filamu ya “Gods must be crazy”, na jina lake kamili ni N!xau na ni maarufu duniani kwa jina la “Bushman”.
2. Ni raia wa Namibia, Hakumbuki tarehe yake ya kuzaliwa na alifariki mnamo mwaka 2003. Alikadiliwa kuwa amezaliwa mnamo mwaka 1943.
3. Aliweza kuhesabu 1 – 20 tu na ndio maana alifuga mifugo ipatayo 20 na hakutaka kuzidisha zaidi ya hapo
4. Ni baba wa watoto 6 na wake 2, na familia yake ipo nchini kwake Namibia.
5. Ameigiza filamu saba (7) ambazo ni The Gods Must Be Crazy (1980), The Gods Must Be Crazy II (1988), Kwacca Strikes Back (1990), Crazy Safari (1991), Crazy Hong Kong (1993), The Gods Must be Funny in China (1994), Sekai Ururun Taizaiki (1996)
6. Katika filamu yake ya kwanza aliambulia kiasi cha shilingi 480,000. kwa sababu katika kijiji chake walichokuwa wakiishi hawakuwa wakitumia pesa na aliona kama hazina umuhimu.
7. Baada ya kufundishwa umuhimu wa pesa ndipo alipoanza kutoza fedha nyingi, katika filamu yake ya pili alitoza fedha ambazo zilimuwezesha kujenga nyumba ya tofali, yenye umeme na maji. (nyumba ya kwanza yenye umeme na maji kijijini kwake).
8. Kabla ya kugunduliwa na “director” Jamie Uys ambaye ni raia wa Afrika kusini, N!xau (Bushman) alikuwa ameowaona wazungu watatu tuu tangu azaliwe.
9. Namibia walimpa jina la utani “mtu maarufu zaidi Namibia” (Namibian most famous).
10. Baada ya kustaafu kuigiza filamu alirudi kijijini kwake ambapo aliendelea na shughuli ya ufugaji na kilimo
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment