Polisi yachunguza chanzo cha moto uliotokea kwenye shule tatu



Polisi nchini Tanzania inachunguza chanzo cha moto uliotokea hivi karibuni katika shule tatu zilizoko kaskazini mwa nchi hiyo.Jeshi la polisi mkoani Arusha linakusanya ushahidi uatakaoonyesha chanzo halisi cha moto huo. Katika wiki moja iliyopita, shule tatu za sekondari mkoani humo ziliwaka moto, huku wanafunzi wakisimamishwa kwa muda.
Bweni katika shule ya sekondari ya Nanja iliyoko wilayani Monduli lilikuwa la kwanza kuwaka moto, likifuatiwa na shule ya sekondari ya Lowassa iliyoko Makuyuni wilayani humo. Shule ya sekondari ya Longido iliyoko wilayani Longido nayo imeingia kwenye orosha hiyo kwa kuchomwa moto hivi karibuni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amesema, polisi bado wanaendelea kuchunguza chanzo na sababu za moto huo.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: