Sehemu Ya 4
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
"lete nijibipu basi"
"mbona kama unaing'ang'ania sana"
"kwani we hujui"
"sijui ndio"
"nataka siku ukiruusiwa, tusiache kuwasiliana"
"apana utanisumbua mbele ya mke wangu"
"jamani dikiii, nipe bwanaaa"
"afu we ni mtu mzima lakini una akili za kitoto"
"kama zako"
"ivi una maana gani kuanza kunirembulia hivyo"
Nilimuuliza huku yeye akiwa amerembua ile mbaya
"kwasababu wewe ni hensam naaaaa unaonekana unayajua, maana nanii yako kubwa"
"afu wewe ni mtu mzima ujue"
"kwani mtu mzima hana tobo"
"ati nini"
"nilisema hivi, ivi sasa hivi mwanamke akivua nguo utamuacha"
ENDELEA............
Nilishangaa sana kwa kusikia maneno ya huyu nesi, maana toka nipate ajali sikuwahi kufanya mapenzi hata siku moja, na dhumuni langu ni kuacha kufanya mapenzi yasio na mpangilio wowote, nilimuangalia sana yule nesi bila ya kumpatia jibu lolote maana nahisi anataka kunirudisha utumwani, kuanzia hapo nilianza kukasirika na kumwambia kua
"samaani dada angu, naomba tueshmiane"
"kwani nimekutukana jamani"
"sitaki maneno yako"
"basi nisamee, ni usichana tu unanisumbua"
"basi kawasumbue wengine ila sio mimi"
Nilikua ni mkali kuliko hata mbwa, maana safari hii sikua nataka mchezo kabisa, coz mapenzi hata uyafanyeje hayaishi bado yapo tu,....... Basi ikiwa ni mwezi wa tatu tarehe za katikati hivi hali iliendelea kuwa nzuri kiasi flani,
BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA
Na sasa ni mwezi wa sita kwenye tarehe za mwanzoni kabisa, mtoto wa kiume nilikua nimeshapona, tena nina afya nzuri kuliko hata mwanzo, mishavu ilijaa hiha mtoto macho yamekua mazuri utafikiri demu, yaani nilikua nina afya nzuri na mwili uliokonda miezi mitatu iliopita, kwa sasa ukiniona huezi nikumbuka tena, kama ulikua kipindi bado nipo hoi hoi nahemea mipira,.... Kunenepa sijanenepa kwahio naomba utofautishe kati ya Afya na Kunenepa, hivyo nilikua nina afya nzuri na nguvu zaidi, sura yangu ilikua imekongoroka sana, lakini kwa sasa imerejea ikiwa inavutia utafikiri toto la mashavuni, kumbe ni choka mbaya,
Baada ya kupona kabisa kabisa yaani hata dozi zote nilishamaliza tena mpaka yule nesi akarudishwa hospitalini kana kwamba zoezi langu limekwisha, ila mbaya zaidi sikua naruusiwa kutoka kutokana na RB nilionayo, maana nikionekana na wale askari heee sidhani kama wataniacha kwakweli, sasa kwakua sikua nikitoka humo ndani hivyo nilikua nikiseidia baadhi ya kazi ndogo ndogo pamoja na kumseidia yule mfanyakazi wa ndani, hata kufagia uwanja, maana ni bonge la mjengo afu lipo ndani ya geti, hivyo nilikua siruusiwi kutoka kabisa japo sikua nikiumwa kwa wakati huo, maana nimeshapona yaani mpaka kwenye kale kachumba cha matibabu siruusiwi kuingia tena, maana hapaniusu kabisa,
Sasa nikiwa naendelea kufanya zangu usafi hapo kwenye gadeni, ghafla mlango ulifunguliwa, kwanza nilimuona mama akiingia, afu wa pili alikua ni mke wangu, dahhh mke wangu kuniona tu alifurahi mno
"waaaaaaooo mume wangu nashukuru kwa kukuona tena, nakupenda sana mume wanguuu"
Jasmini au jasu au mke wangu, alikua akilia kwa furaha ya kuniona nipo hai, maana alikua akiambiwa tu na mama kua nipo hai sijafa, hivyo hakua akiamini mpaka leo ndio siku ya kwanza kuniona toka nipate ajali, sikutaka kum'bembeleza maana alionekana kua na hamu na mimi kuliko chochote kile, Na pia nilishangaa kumuona mke wangu ana uja uzito wa miezi kama minne hivi,... Kumbe siku ile nilipokua nakamatwa aliniambia kua ana mimba ya wiki mbili, na ilikua ni mwezi wa pili hivi, duuuu kweli mke wangu alikua ana mimba, ila sikutaka kumuuliza maana alikua akinililia kwa furaha huku akiwa amekaa kwenye mapaja yangu ...
"shkamoo mamy"
"marahaba hujambo baba"
"sijambo, naaa nadhani kwasasa nahitaji kufanya mazoezi zaidi"
"mwanangu, hayo mazoezi utayafanyia wapi sasa, na unajua kabisa hapo ulipo serikali inakujua umekufa"
"lakini mama, kama vipi twende police nikaombe msamaha kuliko kuishi kimashaka namna hii"
"weeeeeee uende wapi, na ukisubutu kwenda tu, ujue umenifunga mimi mama yako pamoja na dokta na nesi wake"
"kwanini"
"kwasababu mimi nimewadanganya police kua umekufa, na nikamwambia dokta awadanganye kua umekufa, leo hii wakuone upo hai ulizani watatuacha, tena ni kosa la kuidanganya serikali yangu"
"duuuuuuuu, lakini sasa mamy, nitakaa ndani mpaka lini"
"mwanangu sadiki, sina maana ya ukae ndani, nia yangu ni upone kisha nikuhamishe hata uende kenya kwa muda"
"heeeeee huko kwa maalshababu, siendi uko ng'oooo"
"sema basi utaenda wapi"
"mi nataka nikalime tu kijijini"
"hebu nitolee ushenzi wako hapa, ukalime kitu gani, we unajua kulima wewe"
Muda huo tulikua tukijadiliana mimi na mama kua nitaenda kuishi wapi, ili nisionekane hovyo maeneo haya, lakini nia yangu mimi ni kuelekea tanga kwetu, yaani kule wazazi wangu walipozaliwa, lakini mama angu alikua hataki niende tanga kwasababu sintoyaweza maisha ya vijijini, kwahio anahisi nitaenda kuteseka zaidi, lakini kwa mimi binafsi nimeridhia kwenda tanga,
"mamy, mbona maisha ya kijijini ni mazuri tu, tena ukizingatia na huku kujificha jificha ndio kuzuri zaidi kuliko hata huko kenya unapotaka niende"
"mwanangu sadiki, tanga utaenda tu kuteseka baba, maisha ya kijijini yanahitaji moyo kama hukuyazoea"
"mama, huko huko ndio kuzuri, wacha nikalime mama, kuliko niendelee tu kula chakula cha buree"
"mmmhhhh sawa ila mimi sijaridhika kabisa baba"
"mamy, nakuomba uridhike mama angu, maana ukiweka kinyongo sintofanikiwa kwenye mazao yangu"
"ok sawa nimekubali kwa moyo mmoja, ila unaenda na mkeo au"
"nani? Huyo anabaki huku huku"
Mke wangu aliposikia anabaki alishangaaa
"weeeee nani abaki huku, sibaki ng'ooo, twende wote huko huko"
"sasa utaweza kulima wewe"
"nitaweza tu kwani nimezaliwa wapi"
"mama, unamuona mkwe wako alivyo mjeuri ee"
"lakini sadiki, utaendaje mahali umuache mkeo, lazima uende na mkeo"
"sawa mamy but ataenda kulalia wapi"
"kwani wewe unaenda kulalia wapi"
"si kwa bibi"
"na yeye pia huko huko"
"sasa huyu kazoea umeme, je kule kwa bibi kuna umeme sasa"
"weeee nyumba ya bibi ako mimi ndio nilieijenga, ina vyumba sita na umeme umejazana babu wewe, kwahio nenda na mkeo"
Tuliendelea kubishana baina yangu mimi na mama pamoja na mke wangu, maana sikutaka kuenda nae kwasababu ya usumbufu usumbufu wa hapa na pale, tena mke wangu na vile ana mimba duuu ilikua ndio tatizo ambalo sikutaka aende,
"aaaahhh sawa nimekubali kuondoka nae, lakini inatakiwa nitangulie kwanza mimi afu ndio na yeye aje"
"heeeeee kwani wewe unakujua huko kwa bibi yako"
"mmhhh hilo nalo neno, napanga kwenda mahari na wakati sipajui"
"sasa skieni, hapa humuachi mtu, bali keshokutwa nitawapeleka sawa"
"sawa mamy"...........
Maelewano yaliisha na tulipanga tuende kuyaanza maisha tanga kijijini, ambako ndio kwetu kabisa
JAMANI KUSEMA UKWELI, MTUNZI WENU WA STORY ZOTE MLIZO SOMA, NI MZAWA WA TANGA MAENEO YA PONGWE NDIO KWA BABA NA PANGANI NI KWA MAMA, HIVYO KWENYE STORY HII NITACHANGANYA BUT TRUE MIMI NI MTANGA HALISI ILA MBAYA ZAIDI NIMEKULIA NA KUSOMEA ARUSHA HIVYO ZILE SWAGA ZA KIGOSI SINA KABISAAAA..... MAANA HATA KWENDA HUA NI KUSALIMU TU THEN TUNARUDI UBARANI,.....
Baada ya hizo siku mbili mimi nikiwa nipo ndani ya nyumba ya dokta, nikiwa tayari nimeshamuaga kua naondoka ila sidhani kama nitarudi, na pia walishamaliza mkataba wao baina ya dokta na mama, sasa nikiwa nje ya geti la nyumba ya dokta nikiwasubiri akina mama waje twende, Ghafla kweli niliiona ile gari aina ya lamborghine ambayo nilimpa dada aisha pamoja na mama liwe kama usafiri wa kuendea sokoni, yaani gari ya shilingi milioni mianane, eti ni ya kuendea sokoni, ila uzuri ni kwamba gari ilinunuliwa muda kidogo na mama yangu mlezi sonia, maana tulikua na pesa chafu mpaka zinamwagika, hivyo kama ingelikua ni mama yangu huyu asingenunua gari ya gharama kiasi hicho,......
Lakini nilipoangalia vizuri ndani ya hilo gari, nilimuona dada aisha nae yumo, ikabidi nimpigie mama simu
"haloooo, mamy mbona dada aisha namuona kwenye gari"
"sadikiii, kwani aisha kakufanyaje, wacha dada ako akuone hata akupe baraka, yaani majirani wajue umekufa, hata dada yako pia?"
"mamaaaaaaa yaani laiti ungejua ni kwanini namkimbia aisha wala usingesubutu kuja nae"
"we njooo, maana dada yako alikua anaumwa kila siku kisa wewe, na nilipomwambia tu upo hai, yaani ndipo alipopata nafuu"
"hapana bwana mi siji hapo kwenye gari, kama vp nyie nendeni tu"
Unajua kama hukusoma secondary school basi hapa huezi paelewa kabisa, maana hapo ninakataa kwasababu dada aisha nilishawahi kutembea nae kimapenzi wakati hatujuani, sasa tulipokuja kujuana kua ni ndugu lakini dada aisha yeye hataki tuwe ndugu yaani anataka uhusiano uendelee zaidi, na mimi nataka aendelee kujua kua nimekufa ili uhusiano ukate kabisa..... Sasa ndio nashangaa mama kamuambia kua nipo hai,
"unasemaje wewe? Hebu njoo upande twende wewe"
"mamaa mi siji uko"
"sadiki, unajua unanichelewesha we mtoto"
"mamy mi siji, au kama vp mi nitakuja na basi"
"pumbavu wewe hebu njooo haraka mshenzi mkubwa wewe"
Daaaaahhh bimkubwa alimaindi kinoma, ikabidi tu nikubali kwenda,...... Nilifungua mlango wa gari, maana tulipokua tukiongea na mama hatukua mbali ila mimi nilikua nimejificha, hivyo nilijitokeza na kukutana uso kwa uso na dada aisha,.... Na dada nae alianza kunitabasamia huku akitamani kunikumbatia na kunipa denda, ila sema anavumilia kwasababu ya mama,... Niliingia ndani ya gari, kisha nikaketi siti ya nyuma pamoja na yeye aisha,
"shkamo dada"
Nilimsalimia japo kiumbo tupo sawa ila kiumri kanipita, alijitahidi kuitikia huku mimi nimekunja uso.....
Mara mama akageuka, maana yeye ndio dereva,
"sasa nataka mniambie kila kitu kuhusu nyie, ni kwanini mnachukiana, leo niijue hio siri yenu ni ipi"
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment