BYE BYE!!MGOSI ASTAAFU SOKA,APEWA UBOSI SIMBA SC,MKUDE NAHODHA MPYA


Dar Es Salaam,Tanzania.
MSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa klabu hiyo yenye Makao yake Makuu mitaa ya Msimbazi,Dar Es Salaam.
Taarifa ya kustaafu kwa Mgosi imetolewa mchana huu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya URA ya Uganda na itakuwa Live kupitia AZAM TV.
Aidha Manara ameeleza kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu kuanzia leo na Nahodha mpya ni Jonas Gerald Mkude.
Wakati huohuo kiungo wa klabu hiyo, Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC,ametolewa kwa mkopo kwenda klabu ya African Lyon iliyopanda kucheza ligi Kuu msimu huu wa 2015/2016.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: