Wachimbaji wadogo Wa Madini wanaofanya shughuli za Uchimbaji Wa Madini katika Eneo la Kitongoji cha Dodoma Chimboni Kilichopo katika Kijiji cha Amani Kata ya Mundindi wilayani Ludewa hapa Mkoani Njombe wamesema kuwa Wanakabiliwa na Changamoto Kubwa ya Mwingiliano unaojitokeza katika Maeneo ya Uchimbaji Baina yao Kama wachimbaji na Wakulima wanaoendesha Shughuli za kilimo katika wamaeneo hayo.
Siku chache zilizopita wachimbaji hao Akiwemo Bw. Richardi Katemba, Msigwa na Bw. Samweli Kaberege wamesema kuwa Wilaya ya Ludewa inazungukwa na Madini kwa asilimia kubwa hivyo wao Kama wataalamu Wa uchimbaji Hufanya Utafiti katika maeneo mbalimbali Ili kubaini Madini yaliyopo Katika maeneo hayo na Wanapohitaji kuanza Kufanya Kazi ya Uchimbaji Wanaambiwa Maeneo hayo yanamilikiwa na wakulima Hali ambayo inawafanya washindwe kuyafanyia kazi.
Licha ya Kumiliki Migodi mikubwa ya Madini ya Chuma cha liganga katika kata ya Mundindi pamoja na Makaa ya Mawe Yaliyopo katika eneo la Nchuchuma Kata ya Nkomang'ombe Wilaya ya Ludewa pia Inazungukwa Na Maeneo mengi yenye aina mbalimbali za Madini hasa katika Vijiji vya Amani, Ibumi, Njelela, Na Masimavalafu maeneo ambayo Vijana wengi wameshaanza kuyafanyia kazi Ya Utafutaji Maisha Kwa Njia ya Uchimbaji Mdogo Wa Madini Huku wakisema Ndani ya Wilaya ya Ludewa Kuna Madini Aina zaidi ya 120 yenye Thamani Katika Soko La Madini nchini hivyo wameiomba Serikali Kuwatambua na Kuzidi kuwatengea maeneo ya Uchimbaji kwakuwa Kazi hiyo ni kama ajira kwao ,
Kuhusu imani iliyojengeka Kwa jamii kubwa hapa Nchini Tanzania kuhusu Tabia za Wachimbaji wakidhani kuwa wanatabia mbaya katika maisha wanapokuwa Huko Chimboni Wao wanalijibu na kulielezea zaidi Jambo hilo.
Kufuatia Maelezo hayo ya wachimbaji wadogo Wa madini Mwandishi wetu Amefika katika ofisi ya Idara ya Ardhi wilaya ya Ludewa na Kukutana na Bw. Allen Ben ambaye ni Afisa Mipango miji Amesema kuwa Asilimia kubwa ya Wachimbaji wadogo Wa Madini wilayani Ludewa Wanafanya shughuli zao bila kuwa na Leseni za Uchimbaji hali ambayo Hushindwa kusaidiwa pindi wanapohitaji Msaada kisheria Nakuwataka wachimbaji hao wadogo Kuandaa Muhtasari Wa Maandishi juu ya Malaalmiko yao nakuufikisha katika Ofisi yao ya Ardhi kwa Maelezo zaidi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment