Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mohamed Ally
Waziri Professa Mbalawa Akiwapungia Mikono Wananchi wa Kijiji Cha Usalule Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe
Diwani wa Kata ya Ulembwe Agnetha Mpangile Akishukuru Hotuba ya Waziri Mbalawa
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Yusuph Mazana Mwenye Koti la Kijivu Akiwa na Waziri Makame Mbalawa wakati wa Kikagua Barabara ya Njombe Makete
Na Barnabas Njenjema NJOMBE;
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Amesema Serikali Imetenga Kiasi cha Shilingi Trioni 4. Kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Kwa Ajili ya Kutekeleza Miradi ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Barabara Pamoja na Usafiri wa Majini Anga na Reli .
Katika Mazungunmzo Yao na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi , Profesa Mbarawa Amemueleza Mkuu Huyo wa Mkoa Kuwa Katika Fedha Hizo Zitatumika Katika Ujenzi na Ukarabati wa Barabara za Mkoa wa Njombe Zikiwemo zaNjombe Makete, Itoni Ludewa Mpaka Manda , Barabara ya Makambako Mbeya na Pamoja na Barabara ya Kibena Lupembe Hadi Madeke.
Awali Akizungumza na Kujibu Baadhi ya Hoja za Wafanyakazi Pamoja na Wakuu wa Idara Zilizochini ya Wizara Hiyo Profesa Mbarawa Amewataka Watendaji Hao Kufanyakazi Kwa Uadilifu , Huku Akiwashauri Wafanyakazi Hao Kujiendeleza Kielimu.
Mapema Wakitoa Malalamiko Yao Mbele ya Waziri Huyo wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawsiliano Baadhi ya Wafanyakazi Wameelezea Kufanya kazi Kwa Muda Mrefu Bila ya Kupewa Ajira ya Kudumu Licha ya Kuwa Uzoefu wa Kutosha na Badala Yake Wamekuwa Wakifanyakazi Kwa Mkataba wa Muda.
Waziri Mbarawa Amefanya Ziara ya Siku Moja ya Kukagua Baadhi ya Miundombinu ya Barabara Pamoja na Kuzungumza na Watendaji wa Taasisi na Idara Zilizochini ya Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano na Kutoa Maagizo Kwa Watendaji Hao.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbalawa Akielekea Dodoma Baada ya Kuhitimisha Ziara Yake Mkoani Njombe
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment