KOCHA MTUNISIA AONDOKA APR BAADA YA KUWAPA UBINGWA WA NCHI


KOCHA Mtunisia wa APR, Nizar Khanfir ameaga na kuondoka timu hiyo baada ya sherehe za kukabidhiwa ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda Jumapili.
Khanfir aliwaambia Waandishi wa Habari kwamba anarejea nyumbani baada ya Mkataba wake miezi sita kumalizika mwishoni mwa msimu.
“Nilikuwa nina Mkataba wa miezi sita; nitarudi nyumbani kwa sababu kuna majukumu mengine - familia, jamii na kazi. Tunapaswa kufahamu kwamba kila ana matatizo, hivyo nitaendelea kujadiliana na viongozi (wa APR) na kuona kama kutakuwa na mabadiliko, lakini kwa sasa nakwenda nyumbani," alisema Khanfir.
“APR itakuwa bingwa daima. Ninafurahia wachezaji wangu, uongozi na kila mmoja anayehusika na timu. Kila mmoja alifanya kazi yake vizuri hadi kushinda taji hili,” alisema Mtunisia huyo.
Kabla ya sherehe za kukabidhiwa taji hilo, APR ilichapwa mabao 2-1 na mahasimu, AS Kigali katika mechi ya kukamilisha msimu. 
Oneseme Twizerimana na Ernest Sugira waliihakikishia mwisho mzuri wa msimu AS Kigali kwa mabao waliyofunga mapema kabla ya Emery Bayisenge kuifungia timu ya Jeshi la Rwanda bao la kufutia machozi dakika ya mwisho.
APR imemaliza msimu na pointi 67 baada ya mechi 30, ikishinda mechi 21, sare nne na kufungwa tano, ikifunga mabao 43 na kufungwa 18.
Mahasimu wao wakubwa, Rayon Sports, waliomaliza nafasi ya pili wamezidiwa kwa pointi sita na mabingwa, APR, huku Mukuta VS ikimaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake 60, AS Kigali nafasi ya nne pointi 56.
Wakati huo huo Rwamagana City na AS Muhanga zimeshuka daraja baada ya kumaliza mkiani katika ligi ya timu 16.
Wachezaji wa APR wakifurahia na Kombe la Jumapil


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: