LUDEWA JULY 18 NA Barnabas Njenjema
Mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh,Andrea Tsere amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wananchi ambao wanamtazamo hasi katika masuala mazima ya kielimu kuandika barua yenye tuhuma kumi na sita ambazo hazina ukweli ndani mwake dhidi ya mkuu wa shule ya sekondari ya Madunda.
Masikitiko hayo yamejiri baada ya wananchi wasiojulikana kuandika barua yenye tuhuma kumi na sita zinazomkabili mkuu huyo wa shule na kuipeleka barua hiyo kwa waziri mkuu Mh,Kasim majaliwa.
Akizungumza na wananchi zaidi ya mia mbili waliojitokeza kwenye mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoaa wa Njombe Mh,Tsere amemwagza mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Ludewa kuhakikisha wanampata mtuhumiwa huyo haraka iwezekanavyo.
Mh,Tsere amewataka wananchi wilayani humo kufikisha malalamiko yao dhidi ya watumishi wa Umma katika ngazi husika kabla ya kupeleka ngazi za juu ikiwa wana uhakika na tuhuma zinazomkabili mtumishi wa umma.
Mara baada ya mkuu wa wilaya kuzungumza na wananchi hao na kuzitaja tuhuma zilizoainishwa na mtu asiyefahamika aliruhusu wananchi kutoa mawazo na maswali juu ya sakata hilo ndipo wananchi waliposema tuhuma hizo ziko meza kuu wakimtaja Diwani wa kata ya Mawengi Mh,Zembwela Willa.
Kutokana na tuhuma hizo moja ya tuhuma ilisema mkuu wa shule anatumia mali za shule vibaya na hela za serikali pamoja na zinazoletwa na wafadhili.
Barua iliyopelekwa kwa waziri mkuu ilisema kutokana na tuhuma hzo wananchi wa kijiji cha Madunda kata ya Mawengi pamoja na Serikali ya kijiji hicho wameazimia kumhamisha MKUU huyo wa shule ikiwa siyo kweli kutokana wananchi pamoja na serikali ya kijiji hicho kukanusha taarifa hizo kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya uliofanyika July 17 mwaka 2016 shuleni hapo.
Diwani huyo alipoona tuhuma zinaonyesha kuwa ni yeye alisimama na kukanusha kabisha kuwa hajahusika na kumchafua mkuu wa shule ya Sec Madunda kutokana na Dc Tsere kusema kama ni yeye atamshughulikia kikamilifu kwa mkono wa sheria ili iwe mfano kwa wengine.
Naye mkuu wa shule alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema anasikitika saana juu ya tuhuma hizo huku walimu wake wakitoa mchozi kutokana na tuhuma zilizoainishwa kuwa si sahihi ndio chanzo cha walimu kutoa mchozi.
Hata hivyo walimu walisema kama watamhamisha mkuu huyo wa shule na wao wataondoka hali ambayo walimu hao wanadhihirisha kuwa bega kwa bega na mkuu wao katika kuongeza kiwango cha Elimu shuleni hapo.
Wananchi walisema kuwa endapo serikali itamhamisha mwalimu huyo basi shule hiyo itakufa kabisa huku wakiainisha mazuri anayo yafanya MKUU huyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha DivisionI hadi III zinapatkana kwa asimia 90 tofaut na miaka mitano ya nyuma hivyo wananchi hawakuunga mkono juu ya kumtoa mkuu wa shule.
0 comments:
Post a Comment