PADECO YAWANIFAISHA WANANCHI WA LUDEWA KATIKA KUKABILIANA NA UHABA WA MAJI

PADECO YALETA UKOMBOZI UHABA WA MAJI WILAYANI LUDEWA.

Na barnabas njenjema
Ludewa

Wananchi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Luvuyo wakishangilia uzinduzi wa mradi wa maji 

Zahamati ya Luvuyo ikiwa tayari imeshasogezewa mradi wa maji 


 Shule ya msingi Luvuyo nayo imenufaika na mradi huo

Mkurugenzi wa shirika la PADECO Bw.Willbad Mwinuka akifuatilia burudani ya ngoma ya asili katika uzinduzi huo 

 wafadhi wakizindua tenki la maji katika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa



 kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Kongo akiwa na wafadhiri ambao ni Bi.Ines Obieta na Bi.Jimena Frankos

viongozi wa jimbo katoliki la Njombe wakiwa na wafadhiri 

 Mhandisi Zefania Chaula akiongea na wananchi wa Luvuyo



mmoja wa wafadhiri wa mradi huo Bi.Ines Obieta akizindua bomba la maji Livuyo akiwa na mkurugenzi wa PADECO Bw.Willbad Mwinuka 



Diwani wa kata ya Madope Mh.Polycape Mlelwa akiongea na wananchi wa Luvuyo

Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri Ludewa Mh.Mathei Kongo akizindua mradi wa maji katika tenki kijiji cha Luvuyo



Shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu mkoani Njombe ambalo ni shirika la maendeleo shirikishi la PADECO(participatory Development Concern) limekuwa ni mkombozi mkubwa katika kuhakikisha jamii ya Ludewa na vijiji vyake inapata maji safi na salama kwa kujenga miradi ya maji vijijini.

Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi jana ambaye ni kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa katika uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope mkurugenzi wa shirika la PADECO Bw.Willbad Mwinuka alisema kuwa shirika lake lilianza kuutekeleza mradi huo wa maji mwaka 2015 baada ya kubaini kuwa kunauhaba mkubwa wa maji katika kijiji cha Luvuyo.

Bw.Mwinuka alisema kuwa licha ya kufanya mradi huo wa maji katika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope pia shirika la PADECO limefanya miradi ya maji katika vijiji vya Muholo kata ya Luana,Lipangala na Ugera kata ya Mkongobaki pamoja na Maholong’wa kata ya Ludende ambako mradi unaendelea vizuri hivyo ni wazi ahirikala lake limekuwa mkombozi mkubwa katika kupunguza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Alisema kuwa mradi huo ambao umefadhiriwa na shirika la MANOS UNIDAS kupitia jimbo katoriki la Njombe kwa kiasi cha shilingi milioni 186.2 ambapo Halmashauri ya wilaya ya Ludewa imechangia kiasi cha shilingi milioni 32.6 taslimu wakati nguvu kazi ni shilingi 24 milioni wakati shirika la PADECO limechangia kiasi cha shilingi milioni 4 usimamizi taslimu pia wananchi walichangia pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na nguvu kazi katika ujenzi wa mradi.

Bw.Mwinuka alisema kuwa kazi zilizofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa mtego wa maji,tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 75000,vituo 36 vya maji,njia kuu na njia mgawanyo za umbali wa kilomita 19.7 pamoja na chemba za kutolea uchafu na hewa kwani mradi huo ni mkubwa unaweza kusambazwa hata katika vijiji jirani.

“Tumefanya miradi mingi katika wilaya ya Ludewa ya namna hii na imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi kwani hapo awali tatizo la uhaba wa maji lilikuwa ni kubwa na lilisababisha magonjwa ya tumbo na upotevu wa muda kwa akinamama kwa kutafuta maji umbali wa zaidi ya kilomita 7,mahudhurio hafifu kwa wanafunzi hivyo PADECO tumekuwa suruhisho kubwa”,alisema Bw.Mwinuka.

Bw.Mwinuka alisema kuwa upatikanaji wa maji kwa urahisi katika kijiji cha Luvuyo utarahisisha wananchi kufanya kazi za kimaendeleo kama ujenzi wa nyumba bora kwani wataweza kutengeneza tofari karibu na makazi yao pia afya zitaboreshwa na wanafunzi wateweza kuhudhuria masomo yao kwa ufasaha tofauti na awali walitumia muda mwingi katika utafutaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani.

Akitoa hotuba mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo wa maji kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya Luilo Mh.Mathei Kongo alisema kuwa shirikia la PADECO limekuwa mfano wa kuigwa kwani idadi kubwa ya wananchi wa wilaya ya Ludewa wamenufaika na uwepo wa shirika hilo.

Mh.Kongo alisema ni mashirika machache yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakiwafikia wananchi moja kwa moja kwani yako mashirika ya mfukoni ambayo hutumia fedha za wafadhiri kwa kujinufaisha  hivyo aina ya mashirika hayo yanapaswa kujifunza kwa kupitia shirika la PADECO katika utendaji usio na mashaka kuanzia kwa wafadhiri,Serikalini na hata kwa wananchi wenyewe.

Alisema Serikali hasa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa inatambua mchango mkubwa wa PADECO katika kuhakikisha jamii ya wanaludewa inanufaika na miradi ya maji inayojengwa na shirika hilo hivyo yapaswa wananchi kuitunza miundombinu ya mradi huo ili uweze kunufaisha vizazi vilivyopo na vijavyo.

Naye Diwani wa kata ya Madope Mh.Polycap Mlelwa aliupongeza mradi wa PADECO na ule wa Jimbo katoliki la Njombe kwa kuisaidia jamii ya Luvuyo kwani bila kutatua tatizo la upatikanaji wa maji kwa urahisi maisha ya wananchi hao yangeendelea kuwa duni na kuugua magonjwa ya tumbo kila wakati.

Mh.Mlelwa alikiri kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa maji safi na salama katika kata yake hivyo aliwaomba wafadhiri hao kuendelea kuvisaidia na vijiji vingine nyenye mahitaji hayo ambayo imekuwa kero kubwa hasa kwa akina mama kuacha kufanya kazi za kilimo na badala yake kutumia muda mwingi katika kutafuta maji katika mito iliyoko mbali na makazi ya watu.

Aidha akishukuru kwa niaba ya wananchi mmoja wa wananchi wa kijiji cha Luvuyo na mdau wa maendeleo katika kata hiyo Mhandisi Zefania Chaula alisema kuwa ni furaha iliyoje kwa wananchi wa Luvuyo kukabidhiwa mradi wa maji ambao unafanya kazi vizuri kwani haikuwa kazi rahisi kufanikisha kazi hiyo ikizingatiwa umbali wa chanzo cha mradi huo wa maji.

Mhandisi Chaula alisema kuwa ni miaka mingi tokea nchi hii ipate uhuru wananchi hao hawajawahi kupata unafuu wa maji kama ilivyo leo kwani pongezi za dhati ziwaendee wote waliofanikisha mradi huo ambao unafanya kazi vizuri kwani haikuwa kazi rahisi kufanikisha kazi hiyo ikizingatiwa umbali wa chanzo cha mradi huo wa maji.

Aliwataka wananchi kutunza chanzo cha maji hayo kwa kuacha kufanya shughuri za kibinadamu pembezoni mwa chanzo hicho ili mradi huo uweze kuwa endelevu ili mwisho wa siku uweze kuvisaidia na vijiji jirani vyenye uhaba wa maji kama ilivyokuwa kijiji cha Luvuyo.

@habari Ludewa blog

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: