Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye amevitaka vyombo vya habari kuhakikisha kuwa maudhui ya vyombo vya habari yanakuwa kwa asilimia kubwa ya ndani ya nchi.
Akizungumza na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kwenye hafla ya kuwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Maudhui katika ukumbi wa makao makuu ya TCRA Nape amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuzindatia maudhui ya ndani kwa asilimia zaidi ya 60 tofauti na hali halisi ilivyo ya asilimia 60 ya maneno ambayo siyo vitendo.
Amesema kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wadau ikiwemo wasanii kuwa vyombo vya Habari vinazingatia kwa asilimia kubwa maudhui ya nje suala linalopelekea wao kukosa mirabaha.
Naye kiongozi wa maudhui ya utangazaji TCRA Fredrick Ntobi amesema kwamba kwa sasa Mamlaka hiyo inafanya kazi kubwa katika kuchunguza maudhui ya vyombo vya habari na kuvichukulia hatua vyombo ambavyo vinafanyakazi chini ya asilimia 60
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment