HATUA MUHIMU KATIKA MAKUZI YA MTOTO



Katika udadisi wangu nikawa nimepitia kukuta makala hii na nikashidwa kuiacha kwa vile najua wote katika hizi blog lengo letu ni moja kuelimisha jamii.

Hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, kwa nini watu wengine ni walevi? Wengine waongeaji sana? Wengine wakimya sana? Wengine waongo sana? Wengine wana tamaa ya ngono kupita kiasi na kadhalika? Lakini pengine una maswali mengi ya namna hii ambayo yanaonyesha jinsi wanadamu wanavyotofautiana.

Kuna hatua 5 muhimu ambazo mtoto lazima afanye mambo ambayo yanastahili kufanyika katika hatua husika. Na iwapo hayatafanyika, hali hizo huhifadhiwa katika mawazo yake ya kina na hivyo kumsababishia matatizo makubwa ukubwani.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

Hatua ya kwanza – oral stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili. Katika hatua hii ya kwanza, furaha na raha ya mtoto huwa imejificha mdomoni. Utakuta mtoto kila wakati anafurahia kunyonya maziwa ya mama yake, vidole au midoli. Mtoto anatakiwa atumie mdomo wake mpaka ile hamu yake yote iishe. Kama ni kunyonya basi aendelee kufanya hivyo mpaka pale utakapofika wakati mzuri wa kumwachisha ziwa. Kumnyanyasa mtoto wakati ananyonya au kumfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana ikiwa ni pamoja na kumwachisha ziwa mapema, husababisha hamu yake ya kuutumia mdomo ibaki na hivyo kuhifadhiwa kwenye mawazo yake ya kina. Anapokuwa mtu mkubwa hulipa kisasi bila kujua kwa kuutumia mdomo kwa kadri anavyoweza. Hivyo anapokuwa mtu mkubwa anaweza akawa muongo sana, mlevi kupindukia, mvuta sigara sana, muongeaji sana, au mmbeya sana. Kama kuna watu unawafahamu wenye tabia hizi, jaribu kupeleleza kama walinyonyeshwa bila kunyanyaswa au kama hamu yao ya kunyonya iliisha.

Hatua ya pili – anal stage: Hatua hii humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Matumizi ya mdomo huwa yamekwisha na raha huhamia sehemu za haja. Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia au jinsi ya kutumia choo. Kinyume na hivyo ni kumfanya mtoto awe na tabia ya kujifanyisha na hivyo kuwa na hali mbaya ukubwani. Mtoto aliyenyimwa huduma hii akiwa katika hatua hiyo hubakiwa na deni, anapokuwa mkubwa anaweza kupata matatizo ya kiakili. Watoto waliokosa huduma hiyo wanapokuwa wakubwa, mara nyingi huwa mashoga, na wengine huwa waoga kufanya mapenzi, lakini mbaya zaidi ni kukosa kabisa hamu ya mapenzi, wengine huwa wazembe na huwa na tabia fulani fulani ambazo zinahitaji msaada mkubwa wa wengine.

Hatua ya tatu – phallic stage: Hatua hii huwahusu watoto wenye umri wa miaka minne. Ni katika hatua hii ambapo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hivyo kuwa karibu na mama yake au baba yake. Mtoto wa kiume hupenda kulala na mama yake na mtoto wa kike pia huwa hivyo hivyo hupenda kulala na baba yake (interest of opposite sex). Mtoto wa kiume humchukia baba yake bila kujua na kumuonea wivu mama yake na kuona kama anamfaidi baba yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake, pia mtoto wa kike humchukia baba yake na kumuonea wivu baba yake na kuona kama anamfaidi mama yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake. Watoto waliokosa kuwa karibu na wazazi wao wa jinsia tofauti katika hatua hii, wengi hupata matatizo, lakini hulipiza kisasi kwa sababu hawakuwa karibu na jinsia tofauti wanapohitaji kufanya hivyo. Usishangae kumkuta binti akiwa kwenye kundi la wavulana au mvulana akiwa kwenye kundi la wasichana.

Hatua ya nne – latency stage: Hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita, minane na wakati mwigine mpaka miaka 12, ambapo mtoto macho yake yote huwa katika michezo ya kawaida na kwenda shule. Hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika hatua hii kati ya jinsia ya kike na ya kiume.

Hatua ya tano - genital stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13. katika kipindi hiki vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo. Katika hatua hii ndipo mtu hukabiliwa na vitu vingi katika maisha yake yote. Huanza kujishuhulisha na kutafuta maisha yake mwenyewe na ndipo hatua nyingine zote huanza kujirudia tena kama hazikufanywa vizuri katika umri huo. Raha ya mwanadamu yoyote katika kipindi hiki huwa ni mapenzi, lakini hutofautiana kiwango cha kupenda au kutamani kutokana na jinsi alivyolelewa katika hatua nne za mwanzo. Nakuomba sana kila unapokutana na watu waongo, wambeya, wakimya, wapenda ngono kupita kiasi n.k. waulize maisha yao ya utotoni.



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: