Darasa muhimu kwa wagombanao faragha


MUNGU ni mwema kila wakati. Amenikutanisha tena wewe msomaji wangu kwa mara nyingine Jumamosi ya leo ili niweze kuwapa kile nilichokiandaa kwa ajili yako.
MALOVE6
Niwashukuru wote ambao mmenitumia meseji na kunipigia mkipongeza mada ya wiki iliyopita. Leo niwaalike katika mada nyingine ambayo nina amini, ukiisoma kwa umakini hutabaki hivihivi. Mwishoni lazima utakuwa umejifunza kitu kipya!
Ili kukuweka karibu, acha nikupe uhalisia wa mada ya leo. Wengi sana wamekuwa wakilalamika kutodumu katika uhusiano. Wanalalamika pasipo kujua kwamba wao ndiyo chanzo. Wanashindwa kujua kwamba wanapaswa kujisahihisha wao kwanza ili waweze kudumu kwenye uhusiano.
Utakuta mwanamke ana tabia fulani. Ile tabia inawaudhi wanaume wengi. Yeye hajui. Anabaki anajilaumu. Leo anakuwa na mwanaume huyu, anaachika, kesho anahamia kwa mwingine nako anaachika vilevile.
Vivyo hivyo kwa wanaume, utakuta leo mwanaume anakuwa na huyu, anaachika anahamia kwa mwingine, nako pia anaachika. Rafiki yangu, lazima ukubali kujifunza kama unataka kudumu katika uhusiano.
Unapaswa kujua ni wapi unakosea. Ukishatambua kosa lako, lifanyie kazi. Amua kubadilika na utajikuta unadumu kwenye uhusiano. Watu wengi wanashindwa kujua kwamba kuishi na mtu katika uhusiano au ndoa yataka moyo.
Kila mtu anakuwa na hulka yake. Kila mmoja anakuwa amelelewa kwenye malezi tofauti. Ili muweze kuishi pamoja yawapasa kwanza kusomana tabia. Kila mmoja akishajua tabia za mwenzake ni rahisi kusaidiana kubadilishana tabia hususan zile mbaya.
Kila mtu lazima atakuwa na tabia fulani ambayo mwenzake haipendi. Kama kuna kitu hukipendi kwa mwenzako na una uhakika ni kitu kibaya, usisite kumwambia. Tenga muda mzuri. Mwenzako akiwa katika mudi ya furaha, mueleze kuhusu tabia yake isiyokufurahisha.
Mfano; kama mwenzako ana tatizo la kunuka jasho, mueleze na kumpa mbinu stahiki za kuondokana na tatizo hilo. Kama mwenzako anavuta sigara na huwa inakuchefua, mueleze na mshauriane mbinu stahiki za kumaliza tatizo hilo.
Usiwe mtu wa kukataa kila kitu. Usimdharau mwenzako kutokana na udhaifu fulani. Mapenzi ni faragha, faragha ni siri. Usitangaze kwa mtu udhaifu wa mwenzi wako. Shughulika nao mwenyewe. Kumueleza rafiki yako haitasaidia kitu.
Kuachana naye haitasaidia. Utaachana na huyu, utakutana na mwingine naye anakuwa na udhaifu mwingine tofauti. Utakuwa hujatibu tatizo. Utakuwa umebadili tatizo. Dawa ya tatizo si kulikimbia, lishughulike kikamilifu. Tatizo unalolijua ni rahisi kulishughulikia kuliko lile usilolijua.
Umjue mwenzako nini anapenda, nini hapendi. Nini unakifanya kinamkwaza mwenzako? Ukikijua jitahidi kukiepuka. Ikiwezekana usikifanye kama hakina ulazima. Mfano kama unajua mwenzako anapenda kukushika sehemu fulani na wewe hupendi, muelekeze kwa upole ashike wapi pengine ili uendelee kuwa na amani.
Nasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu huwa kama na kisirani hivi. Hawataki kushikwa popote. Kila anapoguswa na mpenzi wake, anasema hataki. Mwenzake anajaribu kubadili kila mbinu ya kumshika, bado haoneshi ushirikiano.
Mbaya zaidi watu wa namna hiyo wanashindwa kutambua kwamba faragha ina nafasi yake. Mtu anakuwa na gugu tu. Hana jema. Akishikwa hapa hataki. Mwenzake akihamia sehemu nyingine hataki. Akibusiwa ndiyo kabisa, eti hataki.
Anamtoa kabisa mwenzake katika mudi ya tendo. Matokeo yake yaweza kuwa kero kwa mwenzake. Kinachofuata hapo ni ugomvi na pengine waweza kujikuta wameachana. Kumbe pengine kama angefanyia kazi udhaifu wake pengine wasingefikia kwenye hatua ya ugomvi.
Faragha inahitaji ushirikiano. Inapokuwa na ushawishi wa upande mmoja, huwa tatizo. Tumieni lugha ya staha kusahishana makosa yenu. Kila mmoja afanyie kazi udhaifu wake kisha kwa pamoja msimamie marekebisho mliyoyafanya na nina hakika penzi lenu litadumu

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: