TRA YAIBUKA TENA TFF KUHUSU KODI, SAFARI HII MAJI YA SHINGO…



TRA
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano ya yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kitita kikubwa cha kodi.
TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.
Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyang’ang’ania magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu za zilizopelekea kufanya hivyo.
“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanatokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.”
“Mpaka sasahivi tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, kodi hizo VAT, pay as you earn, SBL ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu eni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”
Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.
Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: