Gwiji huyo wa soka wa Brazil anaishataki kampuni ya Samsung na anaidai fidia ya dola za kimarekani millioni 30 kwa kosa la kampuni hiyo kutumia taswira yake inayofanana na yake katika moha ya matangazo ya bidhaa zao mpya kwenye magazeti – bila kuwa na makubaliano nae ya kimkataba, wanaripoti Financial Times .
Tangazo ambalo limeleta mashtaka haya limetokea katika gazeti la The New York Times mwezi Oktoba mwaka jana japo halitoi picha ya moja kwa moja mtu aliyetumika kwenye tangazo hilo ni Pele..
Hata hivyo kwa mujibu wa mwanasheria wa mwanasoka huyo amesema picha iliyotumika inayofanana mno na mteja wake pia wameongezea taswira nyingine ya mchezaji akipiga “modified bicycle or scissor-kick, staili ya upigaji mpira ambayo Pele alikuwa akiitumia sana.
Samsung wamewahi kuwa na mazungumzo na Pele ya kutumia taswira yake tangu mwaka 2013, lakini mazungumzo hayo yalivunjika na Samsung wakokosa haki ya kisheria kutumia taswira ya Pele kwa namna yoyote.
Mpaka sasa Samsung wamegoma kuzungumzia suala hili walipotafutwa na vyombo vya habari.
Malalamiko ya Pele yaliyowasilishwa na mwanasheria wake Frederick Sperling yaliongeza – kwamba tangazo la Samsung linaenda kinyume na haki za kisheria alizonazo Pele – matangazo ya biashara ni sehemu ya kipato anachotegemea mwanasoka huyo mstaafu.
Pelé mpaka sasa ana mikataba kadhaa ya kutangaza bidhaa za makampuni kama Subway, Volkswagen, na Emirates. Kwa maaka 2015 tu alivuna kiasi cha dola million 25.
Mwanasheria Sperling huko nyuma aliwahi kumsaidia mcheza basketball Micheal Jordan kushinda kesi ya $8.9 million dhidi ya supermarket za Dominick baada ya kumtumia Jordan kwenye matangazo yao bila haki ya kimkataba.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment